Thursday, 22 September 2016
Faida za kunywa maziwa fresh katika miili yetu
Maziwa yana faida nyingi sana kwa afya zetu japo wengi wetu hatuna tabia ya kunywa maziwa ima kwa kuyakosa au kutojua faida zake,na sababu hii ya pili imekusanya watu katika jamii,wengi wetu huacha kutumia kitu fulani kwa kutojua thamani au faida zake,
Zifuatazo ni faida zinazopatikana katika kunywa maziwa;
Kuboresha afya ya ngozi zetu na kuzifanya zionekane ng'aavu,na nyororo zenyekuvutia
Huyapatia macho uimara wa kuona hasa wakati wa usiku au kwenye mwanga hafifu kwa kuwa yana Vitamin A yenye mchango mkubwa katika uoni na kukosekana kwake huenda kukasababisha upofu
Kuusaidia mwili kufyonza madini ya kalsiam<calcium>
madini ya kalsiam yana umuhimu sana katika miili yetu ili kuboresha afya ya mifupa,hasa kwa wajawazito na watoto,na pia madini haya hutumika katika mtandao wa ufahamu<Nerve Conduction> mwilini
ila mwili huyatoa nje madini haya kwa kuyaona kama hayahitajiki,na hapa ndipo unapokuja umuhimu wa kunywa maziwa kwani yana Vitamin D ambayo husaidia mwili kufyonza kalsiam na kuufanya husiyatoe nje madini ya kalsiam<Calcium>ambayo pia hutumika katika misuli<Muscles>wakati wa kujikunja na kujikunjua
maziwa yana madini muhimu yanayohitajika mwilini kama vile Salfa,Phosphoras na Sodium ambayo hutumiwa na mwili katika kazi mbalimbali
Na hutupatia protini<Protein>ambayo huujenga mwili na kuufanya ukuwe vizuri.
Labels:
MWANZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment