Monday, 26 September 2016

Wanafunzi watisha kuzua ghasia Afrika Kusini

Vyuo vikuu kadha vilifungwa baada ya kuzuka ghasia za wanafunzi
Kiongozi wa wanafunzi katika chuo cha Witwatersrand nchini Afrika Kusini ameonya kuwa wanafunzi watavuruga shughuli zote nchini humo ikiwa matakwa yao ya kupewa elimu ya bure hayatatimizwa juma hili.
Onyo la kiongozi wa baraza linalowakilosha wanafunzi Kefentse Mkhari, linatolewa baaada ya maandamano yenye ghasia kuzuka kwenye mji mkuu Johannesbug wiki iliyopita, baada ya serikali kutoa pendekezo kuwa itaongeza karo kwa hadi asilimia nane mwaka ujao.

"Kwa sasa tunataka elimu ya bure na kama serikali haitajitolea kutupa elimu ya bure , basi tutaifanya nchi hii isitawalike,"alisema Mkhari.

No comments:

Post a Comment