Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir
Ujumbe wa nchi hiyo uliongozwa na Mshauri Mkuu wa Uchumi wa Rais wa Sudani Kusini, Aggrey Tisa Sabuni ambaye alimkabidhi mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC Balozi Augustine Mahiga ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa .
Waziri Mahiga alisema kuwa Sudani Kusini imekua mwanachama kamili sawa na wanachama wengine watano na Septemba 8 mwaka huu, Rais wa nchi, Salva Kiir hiyo atahudhuria mkutano wa dharula wa wakuu wa EAC utaongozwa na mwenyekiti wake Rais John Magufuli jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment