Monday, 5 September 2016

Heshima ya Samatta ndani ya KRC Genk inazidi kupanda kila kukicha

Heshima ya mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta inazidi kupanda tartiiibu katika kikosi chake cha KRC Genk cha nchini Ubelgiji.
Heshima ya Samatta imezidi kupanda kutokana na namna ambavyo amekuwa akifunga mfululizo.

Kabla, haikuwa rahisi kuona Samatta akiwekwa kwenye matangazo ya kikosi hicho. Lakini sasa tayari ana mabao manne, hali inayomfanya Genk waone ni kati ya wachezaji wao muhimu.

Katika matangazo mengi kuhusiana na mechi za Genk au mambo mengine muhimu, Samatta amekuwa akitumika, kitu ambacho awali ilikuwa aghalabu.


Kutumika kwenye matangazo ni sehemu ya kuonyesha una mvuto au unakubalika. Jambo ambalo ni bora kwa Samatta na anachotakiwa ni kuongeza tu juhudi.

No comments:

Post a Comment