Monday, 5 September 2016

Steve Nyerere atangaza kuoa Januari

Msanii mkongwe wa filamu Steve Nyerere aliwasurprise baadhi ya wasanii wenzake wa filamu katika harusi ya Shamsa Ford baada ya kutangaza anaoa mwezi januari mwakani.
Akitoa neno kwa niaba ya wasanii wenzake katika harusi ya Shamsa Ford iliyofanyika Sinza Afrikasana Ijumaa iliyopita, Steve Nyerere aliwaabarisha wasanii wenzake kuwa ataoa Januari 2017.
“Mimi sina maneno mengi yakusema zaidi ya kuwapongeza na kuwaombea muishi salama, pia mungu akipenda na mimi nitafunga ndoa Januari,” alisema Steve.

Baada ya kusema kauli hiyo, kuliibuka shangwe kutoka kwa wasanii ambao walihudhuria ndo
a.

No comments:

Post a Comment