Sunday, 20 August 2017

Watu zaidi ya 15 000 waandamana kupinga ubanguzi wa rangi Boston

Watu  zaidi ya 15 000 waandamana kupinga ubanguzi wa rangi Boston
Watu zaidi ya 15000 wameandamana mjini Boston nchini Marekani kupinga mkutano wa hadhara wa wafuasi wa mrengo wa kushoto ambao umetuhumiwa kuzagaza sera za kibaguzi.
Maandamano hayo yameandaliwa siku kadhaa baada ya ghasia zilizotokea  Charlottesville ambapo mtu mmoja alifariki na wengine kujeruhiwa baada ya mfuasi wa mrengo wa kulia kugonga umati wa watu waliokuwa wakiandamana.
Mashirika ya kibinafsi yalitoa wito wa maandamano kupinga mkutano wa hadhara  wa wafuasi wa  mrengo wa  kulia ambao unadai kutetea uhuru wa kujieleza.

Mashirika hayo yanasema kuwa uhuru wa kujieleza sio kuvuka mipaka kkwa ubaguzi wa rangi
.

No comments:

Post a Comment