Waziri Ummy Mwalimu
akizungumza na watumishi wa hospitali inayomilikiwa na Kanisa ya
inayoitwa Dkt.Artiman iliyopo manispaa ya sumbawanga,kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Sumbawanga Dkt.Khalfan Haule na kuliani ni Afisa Tawala wa
Mkoa wa Rukwa Bernard Makali
WAMJW-Rukwa
Viongozi wa Mkoa wa Rukwa
wametakiwa kusimamia fedha za dawa pamoja na upatikanaji wa dawa katika
vituo vyote vya kutolea huduma za afya vilivyopo kwenye mkoa huo
Waziri wa Afya,naendeleo ya
Jamii ,Jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo jana wakati
akiongea na viongozi na watumishi wa Wilaya na mkoa wakati wa
kuhitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani hapa
“Nahitaji mfamasia awe
anaprinti karatasi yenye kuonyesha dawa zilizopo kwenye stoo yake ili
mganga anayeingia zamu siku hiyo aweze kujua dawa zilizopo na
kumuandikiamgonjwa wake kuliko kuanmdika dawa ambazo hazipo kituoni hapo
Aidha Waziri Ummy aliwapongeza
mkoa huo kutokana na kuwa na hali nzuri nya uwepo wa dawa katika vituo
vyote alivyotembelea ingawaje bado kuna changamoto ya utoaji elimu kwa
wananchi kuhusu uchangiaji wa dawa na kuwataka wakimaliza dawa
walizonazo stoo zikiisha wanatakiwa kupunguza bei za dawa ili wananchi
waweze kupata dawa hizo pasina shaka
“Mheshimiwa Rais alisema hataki
kuona wananchi wanapata shida ya upatikana wa dawa kwenye vituo vya
kutolea huduma vya serikali hivyo akaongeza bajeti ya dawa kwa miaka
miwili mfululizao”akitolea mfano kwa mkoa wa Rukwa ,mwaka 2016/2017
bajeti ya dawa iliongezeka kutoka milioni 495 hadi kufikia bilioni 1.4
na kwa mwaka huu 2017/2018 imeongezwa na kufikia bilioni 2.02.
Hata hivyo alisema upatikanaji
wa dawa huo utaongezeka kutokana na kwamba hivi sasa serikali kupitia
bohari ya dawa(MSD) inanunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji
wa ndani tofauti na zamani ambapo walikua wakinunua toka kwa mawakala
Waziri Ummy aliwapongeza Mkoa
huo licha ya changamoto zote zinazowakabili katika vituo vya kutolea
huduma bado mkoa huo unasonga mbele katika kukabiliana na tatizo la vifo
vitokanavyo na na uzazi kwa vifo 117 kati ya vizazi hai laki moja
wakati takwimu za kitaifa ni vifo 506
Kwa upande wa vifo vya watoto
chini ya miaka mitano wamepunguza na kuwa na vifo 31 kati ya vizazi hai
laki moja ambapo takwimu za kitaifa ni 67,aidha kwa akina mama
wajawazito wanaoenda kujifungulia kwenye vituo vya afya mkoa wa Rukwa ni
akina mama 65 kati ya mia moja ambapo takwimu za kitaifa ni akina mama
64,’hapa niwapongeze mmepiga hatua sana’
Kutokana na jitihada za
serikali za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya
miaka mitano hivi karibuni ilinunua na kusambaza kwenye halmashauri zote
vitanda ishirini na tano ikiwemo vitanda vitano kwa ajili ya
kujifungulia pamoja na mshuka hamsini
Awali Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mhe.Justine Haule
aliishukuru Serikali kwa kuwapatia vitanda pamoja na mashuka na hivyo
kupunguza changamoto ya vitanda katika wodi za akina mama wanaojifungua
na alitaka changamoto kubwa ni kwamba mji wa rukwa unaendelea kukua
hivyo bado huduma za afya zinahitajika sana ili kuweza kutoa huduma bora
kwa wananchi
No comments:
Post a Comment