Meneja Mwandamizi Kitengo cha
Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto) akizungumza
kabla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya mchezo wa mpira wa miguu kwa
ajili ya Timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Daraja la Kanza
Tanzania Bara. Wengine kushoto kwake ni maofisa waandamizi wa Jeshi la
Polisi Tanzania walioshiriki kupokea vifaa hivyo vya msaada
Meneja Mwandamizi Kitengo cha
Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto) akizungumza
kabla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya mchezo wa mpira wa miguu kwa
Timu ya Polisi Tanzania inayotarajia kushiriki Ligi Daraja la Kanza
Tanzania Bara. Kulia ni Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmada Khamis
wakishuhudia tukio hilo.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha
Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto) akimkabidhi
baadhi ya vifaa vya michezo Naibu Kamishna wa Polisi, Adrian Magayane
(kulia) vilivyotolewa na NMB kwa ajili ya Timu ya Polisi Tanzania
inayoshiriki Ligi Daraja la Kanza Tanzania Bara. Wengine katikati kutoka
kushoto ni Kaimu Afisa Mwandamizi Amana, Huduma za Bima na Huduma za
Ziada wa NMB, Stephen Adili na Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmada Khamis
wakishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya
NMB (kushoto) pamoja na wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa katika picha
ya pamoja mara baada ya zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lililofanyika leo
jijini Dar es Salaam, Makao Makuu ya Benki ya NMB. Vifaa hivyo
vimetolewa na NMB kwa ajili ya Timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi
Daraja la Kanza Tanzania Bara.
Sehemu ya Maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imekabidhi msaada
wa vifaa mbalimbali vya mchezo kwa Timu ya Mpira wa Miguu ya Jeshi la
Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Vifaa hivyo ni pamoja na
mipira, mabegi ya wachezaji, viatu, tracksuit na jezi mbalimbali vyote
vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13, vilikabidhiwa kwa jeshi la
polisi na Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB – Ally
Ngingite kwa Kamishna wa Polisi – Adrian Magayane.
Akizungumza kabla ya kukabidhi
vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, bwana Ngingite alisema NMB
inaamini msaada huo kwa Timu ya Jeshi la Polisi utakuwa chachu ya
kufanya vizuri zaidi katika michuano mbalimbali iliyopo mbele yao
hususani Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara inayotarajia kuanza hivi
karibuni.
“Vifaa tunavyokabidhi leo ni
pamoja na jezi, track suti, mabegi, mipira, viatu vya kuchezea na vifaa
vingine vingi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13,” alisema
bwana Ngingite
Msaada huo kwa timu ya jeshi
la polisi ni mwendelezo wa kusaidia kukuza sekta ya michezo nchini huku
benki hiyo ikijinasibu kuwa imekuwa mshirika mkubwa sana katima
maendeleo ya michezo nchini. Mbali na kuisaidia timu ya polisi, NMB pia
inaidhamini timu ya Azam MC ya Ligi Kuu Tanzania Bara na imekuwa
ikisaidia timu mbalimbali kuendeleza michezo.
Bwana Ngingite alizitaja timu
nyingine ambazo NMB imetia Mkono wake hapa nchini ni pamoja na clabu ya
Gofu ya Lugalo, Singida United na Clabu ya jeshi ya Gymkana.
Akiongea baada ya kupokea
vifaa hivyo, Kamisha wa Polisi – Adrian Magayane alishukuru kwa msaada
na kusema kuwa utaongeza chachu ya ushindi na kuhakikisha kuwa wanatinga
ligi kuu msimu ujao.
“Tunawashukuru sana NMB, benki hii
imekuwa mshirika wetu mkubwa sana katika nyanja mbalimbali, tunaimani
tutabeba nembo yao vizuri kwa kufanya vyema kwenye mashindano ya ligi
daraja la kwanza.” Alisema Kamishna Magayane.
No comments:
Post a Comment