Saturday, 5 August 2017

Samatta apewa kadi ya njano

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Champion Boy’ usiku wa Ijumaa alionyeshwa kadi ya njano timu yake, KRC Genk ikifungwa mabao 2-1 na wenyeji, Standard Liege katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege.
Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo katika mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu ya Ubelgiji, Genk ikicheza bila kushinda baada ya Jumamosi iliyopita kulazimishwa sare ya 3-3 na Waasland-Beveren Uwanja wa nyumbani, Luminus Arena.
Samatta jana alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 41 ikiwa ya tano tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kisemokrasia ya Kongo (DRC) na bahati nzuri kwake hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu.
Mbwana Samatta jana ameonyeshwa kadi ya njano timu yake, KRC Genk ikifungwa mabao 2-1 na Standard Liege
Katika mchezo huo, Genk walitangulia kupata bao, lililofungwa na mshambuliaji kinda wa miaka 21, Siebe Schrijvers dakika ya 36, kabla ya kiungo Mbrazil Edmilson Junior kuwasawazishia wenyeji dakika ya 48 na mshambuliaji Mkongo, Paul-Jose M'Poku Ebunge kufunga la ushindi dakika ya 63.
Huo unakuwa mchezo wa 57 kwa Samatta katika mashindano tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk, kati ya hiyo mechi 34 alianza na mechi 21 alitokea benchi.
Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar e Salaam, amefunga jumla ya mabao 19.

Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Vukovic, Maehle, Brabec, Colley, Khammas/Nastic dk55, Berge, Heynen/Ingvartsen dk69, Writers, Buffalo/Malinovskyi dk80, Trossard na Samatta.

Standard Liege Setup: Ochoa, Agbo/Marin dk45, Dossevi, Scholz, Pocognoli, Bope, Fai, Edmilson, Laifis, Mpoku/Kosanovic dk83 na Sa.

No comments:

Post a Comment