Thursday, 3 August 2017

Rais Magufuli aliamuru Jeshi kurudisha ardhi.

 Image result for john magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amelitaka Jeshi kurudisha eneo ambalo wameshindwa kuliendeleza, ili wananchi waweze kulitumia kwa shughuli za kilimo.
Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Handeni mkoani Tanga ambako ameenda kwenye uzinduzi wa bomba la mafuta la HOIMA, amesema kama Jeshi limeshindwa kuendeleza eneo hilo, ni vyema walirudishekwa wananchi ili waweze kulitumia kwa kilimo.

" Nimeambiwa kuwa Mgambo JKT walipewa eneo la hekari 50 kwa ajili ya kujenga kiwanda, hawajajenga tangu wapewe, naomba eneo hilo lirudishwe, kama Jeshi wameshindwa kulitumia ardhi hiyo na kuiendeleza, ni bora wairudishe kwa wananchi walime, Mbunge naomba lisimamie hilo kwa sababu ulinieleza kuna tatizo la ardhi, eneo hilo lilichukuliwa miaka 7 sasa hawajaliendeleza maana yake hawana uwezo wa kuliendeleza, wanakijiji wanalihitaji kwa kulima huko", alisema Rais Magufuli.


Akiwa njiani Rais Magufuli alisimama katika eneo la Mkata Handeni mkoani Tanga na kusikiliza kero za wananchi, na kukutana na malalamiko hayo ya ardhi pamoja na ukosefu wa maji.

Rais Magufuli anatarajiwa kuzindua ujenzi wa bomba kubwa la kusafirissha mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanzania, siku ya tar tar 5 Agosti 2017.

No comments:

Post a Comment