Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Kampuni moja ya data ya mitandaoni iliomfanyia kazi Donald Trump na ambayo ilitumika katika kampeni za Brexit sasa imeripotiwa kumfanyia kazi rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Lengo la Cambridge Analytica ni wazi. Katika Mtandao wake kampuni hiyo inasema inatumia data kubadili tabia ya wateja wake.
Kampuni hiyo iliokodishwa na kundi la kampeni za rais Trump imepongezwa kwa ushindi wa rais huyo.
Kampuni hiyo inanunua na kukusanya data kuhusu wapiga kura ikiwemo historia ya utumizi wao wa mtandao, mahali walipo pamoja na 'Likes' zao {wanachopenda} katika mtandao wa facebook.
Katika mtandao wake, Cambridge Analytica inadai kukusanya maeneo 5,000 ya data miongoni mwa wapiga kura milioni 320 wa Marekani.
Zinapochanganywa pamoja na utafiti unaofanywa , Cambridge Analytica inaweza kutumia data hiyo kutoa ujumbe muhimu kwa wapiga kura.
Kwa sasa Cambridge Analytica inafanya kazi Kenya , ikisaidia juhudi za kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru kenyatta.
Mnamo mwezi Mei , gazeti la The Star nchini Kenya liliripoti kwamba Chama cha rais Kenyatta, Jubilee kimekodisha kampuni hiyo , na mwezi mmoja baadaye ,gazeti hilo hilo liliripoti kwamba Cambridge Analytica ilikuwa ikifanya kazi katika ghorofa ya 7 ya jumba la makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi.
Cambridge Analytica ilikataa kutoa tamko lolote kuhusu ripoti hizo kwa kitengo cha habari cha BBC Trending, lakini shirika la Privacy International lilithibitisha kwamba liliona habari kama hizo katika gazeti la The Star kufuatia duru kadhaa, na kusema kuwa Cambridge Analytica inalipwa dola milioni sita kwa kazi yake nchini humo.
No comments:
Post a Comment