Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga
akizungumza na wadau wa Asasi za Kirai nchini na Waandishi wa Habari
Mjini Dodoma katika uzinduzi wa uhakiki wa Asasi za Kiraia Agosti
21,2017.
Msajili wa Asasi zisizokuwa za
kirai Bw. Marcel Katemba akisisitiza jambo kuhusu mwitikio chanya
uliooneshwa na mashirika hayo katika uandaaji wa uhakiki wa Mashirika
Yasiyokuwa ya Kiserikali katika kikao na waandishi wa habari mkoani
Dodoma Agosti 21,2017.
Mwenyekiti wa Baraza la Asasi za
Kiraia Tanzania Bw. Nicholous Zakaria akipongeza azma ya Seriklai
kuendesha uhakiki wa mashirika yasiyokuwa ya kireikali katika kikao cha
uzinduzi wa zoezi hilo mkoani Dodoma Agosti 21,2017.
Mwenyekiti wa Maandalizi ya
Uhakikiki wa Asasi zisizokuwa za Kiserikali Bw. Onesmo Olenguruma
akielezea kuridhishwa na ushirikishwaji wa Mashirika Yasiyokuwa ya
Kiseriklai katika kuendesha uhakiki wa mashirika hayo hapa nchini Agosti
21,2017.
Katibu Mkuu Baraza la Asasi za
Kiraia Tanzania Bw. Ismail Suleiman akisisitiza kuendeleza mashirikiano
katika kufanikisha uhakiki wa mashirika yasiyoya kiserikali ambao katika
kiako cha uzinduzi kilichofanyika mkoani Dodoma Agosti 21,2017.
Baadhi ya wadau kutoka Asasi za
Kirai nchini, watendaji wa Wizara na waandishi wa Habari wakimsikiliza
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
Bibi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa uhakiki wa
mashirika yasiyo ya kiserikali uliozinduliwa mkoa Dodoma Agosti 21,2017.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akiwa
katika picha ya pamoja na wadau wa asasai zisizo za kiserikali muda
mfupi baada ya uzinduzi wa kazi ya uhakiki wa mashirika hayo hapa nchini
Agosti 21,2017.
Picha na Erasto Ching’oro WAMJW
Na Raymond Mushumbusi WAMJW
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amewashauri
wamiliki wa Asasi za kiraia (NGOs) kutumia fursa ya muda uliotolewa na
Wizara kuhakiki asasi zao na wale ambao hawajasajili asasi zao
kuzisajili.
Ametoa ushauri huo leo Mjini
Dodoma wakati akizindua mpango wa kuhakiki Asasi zisizo za kiraia
unaoanza Agosti 21, 2017 na kumalizika Septemba 4, 2017.
Ameongeza kuwa suala la kuhakiki
Asasi za kirai ni la muhimu na litapelekea kupata kubaini asasi hizo
nchini na mchango wao kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
“Niyaombe yale mashirika ambayo
yanafanya kazi za NGO’S na hayakusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya NGOs
yatumie fursa hii kujisalimisha na kujisajili’’ alisema Bibi Sihaba.
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti
wa Baraza la Asasi za Kiraia Tanzania Bw. Nicholous Zakaria ameishukuru
Serikali kwa kuchukua hatua nzuri ya kuhakiki Asasi hizo ili kupata
taarifa zilizo sahihi kuhusu asasi hizo kwa maendeleo ya asasi, jamii na
taifa kwa ujumla.
“Nichukue fursa hii kuipongeza
Serikali kwa ushirikiano mnaotupatia kupitia Waziri, Katibu Mkuu na
Msajili wa Asasi za kiraia katika kufanikisha shughuli zetu za kila
siku” alisema Bw. Nicholous Zakaria.
Katika kuhakikisha zoezi la
uhakiki linafanikiwa na kuwafikia wadau wengi zaidi Wizara imegawa
uhakiki katika Kanda tano ambazo ni Kanda ya Mashariki itakayohudumia
mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Morogoro na Pwani, Kanda ya Kati
itakayohudumia mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida, na Dodoma, kanda ya
Ziwa itakayohudumia mikoa ya Geita, Shinyanga, Mara, Kagera na Mwanza,
Kanda ya kasikazini itakayohudumia mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro
na Tanga, Kanda ya Nyanda za Juu itahudumia mikoa ya Katavi, Rukwa,
Ruvuma, Njombe, iringa na Mbeya.
Aidha, mmiliki wa asasi
anaweza kupata huduma ya usajili katika kituo kitakachokuwa karibu ili
kufanikisha zoeezi la uhakiki ambalo litatoa sura halisi ya idadi,
shughuli na mchango wa kisekta katika maendeleo ya Taifa.
No comments:
Post a Comment