Tuesday, 22 August 2017

Msigwa amvaa Msukuma

Mbunge wa Iringa mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa ameibuka na kumchana Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku na kusema uelewa wake juu ya hoja za Mwanasheria Tundu Lissu ni mdogo sana.
Msigwa amesema haya siku moja baada ya Mbunge Msukuma kudai kuwa yeye anaunga mkono kauli ya serikali kuhusiana na wanasiasa kuchochea sakata la ndege huku akiwatuhumu kuwa wapinzani wanatafuta kiki na kusema ni waongo watupu.
"Msukuma anasukumwa na uelewa Mdogo wa mambo ya kisheria na kimataifa kwa uelewa wake juu ya hoja za Tundu Lissu ni sawa na kobe kushindana na twiga kwa uwezo wa kuona Mbali" alisema Peter Msigwa
Aidhaa Mchungaji Msigwa ameitaka serikali kutoa majibu yanayoridhisha kuhusiana na ndege inayoshikiliwa nchini Canada
"Hoja zilizotolewa na Serikali juu ya kukamatwa kwa ndege yetu huko nchini Canada Bombadier Q 400 zinafedhehesha Taifa na kuondosha weledi na umahiri wa Serikali katika kukabiliana na maswala makubwa ya nchi yetu. Kinachoshangaza Serikali badala ya kujibu hoja kuntu za Mh, Lissu imeendeleza kufanya mazengaombwe yasioleweka kwa watanzania ikisaidiwa na Msukuma mbunge wa Geita. Mpaka sasa Serikali haijatoa majibu ya kuridhisha kuhusiana na sakata hili" alisisitiza Msigwa
Mchungaji Msigwa ameeleza kuwa serikali inapaswa kuja na majibu katika hoja kadhaa ambazo Tundu Lissu aliziibua

"Lissu anawataja wanasheria wa serikali kutowajibika katika kuishauri serikali kinyume na taaluma zao . Watu hawa wamekuwa hawana Masada kwa Serikali wamekuwa wakiingiza mkenge Serikali kila mara na siwashangai kina Prof. Kabudi , Dr. Mwakyembe mithili ya Dr. Benson Banna ambae kila siku amekuwa akiidhalilisha taaluma ya wasomi.

"Serikali mpaka sasa , haijawapa watanzania uhakika ni kwa namna gani mali za watanzania ikiwemo majengo ya balozi zetu zilizopo nje ya nchi zitakuwa salama . Watanzania wanataka majibu yenye uhakika juu ya mali zao kuendelea kunaswa huko nje" alimalizia Peter Msigwa

No comments:

Post a Comment