Wednesday, 16 August 2017

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya aunda kamati kuchunguza moto soko la Sido



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, ameunda kamati ya kufanya tathmini kujua hasara na chanzo cha moto uliotokea usiku wa kuamkia jana katika Soko la Sido, lililoko Mwanjelwa mjini Mbeya.
Pamoja na mambo mengine, Makalla ametoa pole kwa wafanyabiashara wa soko hilo kwa kuharibiwa mali zao na moto huo.
“Soko la Sido lilianza kuungua saa tatu usiku wa kuamkia leo na kuteketeza mali  za wafanyabiashara wa soko hilo, pamoja na kutoa pole niwashukuru wananchi, vyombo vya ulinzi kwa ushirikiano na kazi kubwa ya kudhibiti moto usiendelee kuleta madhara  makubwa zaidi.
“Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Mbeya imeunda kamati, naomba wananchi waendelee kuwa watulivu na watoe ushirikiano kwa kamati hiyo ili tuweze kujua chanzo cha moto na hasara iliyopatikana,” amesema Makalla.

Hata hivyo, baadhi ya wafanyabisahara wamedai moto huo ni hujuma ili kuwafanya waende katika Soko la Mwanjelwa walilotengewa na serikali ambalo wanadai jiografia yake haijakaa vizuri kibiashara.

No comments:

Post a Comment