Christopher Wray
Washington.Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya
kumthibitisha Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Kijasusi la Marekani la FBI.Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu James Comey alipoondolewa kwenye wadhifa huo na na Rais Donald Trump Mei.
Aliondolewa baada ya uchunguzi aliokuwa akiufanya kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo uliompa ushindi Trump.
Christopher Wray ni mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa mahakama ya nchi hiyo ambaye amefanya kazi chini ya Rais George Bush.
No comments:
Post a Comment