Monday, 7 August 2017

Lissu amvaa Waziri Mwijage kuhusu kujiari kwa vijana

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu amefunguka na kumchana Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage kuwa anahamasisha vijana kujiajiri wakati yeye analialia.
Mh Tundu Lissu amesema hayo baada ya kuona video ya Waziri Mwijage akisema kuwa yeye anaipenda sana kazi yake ya Uwaziri na kusema watu ambao wamepewa viwanda wasitake kumponza akapoteza nafasi hiyo.
"Niwaambie watu wote mniepushe na kikombe hiki wote mliopewa viwanda kwa bei ya kutupwa nimepewa amri hivyo viwanda vifanye kazi, naomba msiniponze nina watoto na hii kazi ninaipenda" alisikika Waziri Mwijage.
Baada ya kuona video hiyo Mh Tundu Lissu anasema kuwa mawaziri mbalimbali wamekuwa vinara kuhubiri majukwani na kuwahamasisha vijana waliomaliza vyuo mbalimbali kwamba wanatakiwa kujiajiri wakati wao wenyewe wameshindwa kufanya hivyo. 

"Waziri analia kuwa ni yatima, ana watoto, anaipenda kazi, Majukwanii wanahamasisha vijana waliokopeshwa fedha za kugharamia masomo wajiajiri" alisema Tundu Lissu.
Jana Rais Magufuli amemsifu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa kuanzisha viwanda mbalimbali lakini amesema kuwa anachukizwa na Waziri huyo anapokuwa mzito kufanya maamuzi ya kupokonya viwanda mbalimbali ambavyo havifanyi kazi na kusema sasa anataka kusikia watu wakinyang'anywa viwanda hivyo.

No comments:

Post a Comment