Monday, 21 August 2017

Heche awavaa wasomi wanaohoji uzalendo wa Lissu

Mbunge John Heche 
Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), John Heche amefunguka na kuwachana baadhi ya wasomi wa nchi na serikali ambao awali waliibuka na kudai Tundu Lissu amehongwa na wazungu na kusema uzalendo wa nchi si kuiunga mkono serikali.
John Heche amesema hayo baada ya baadhi ya wasomi kuibuka na kuanza kumtuhumu Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu huku wakisema kuwa kiongozi huyo si mzalendo wa nchi hii huku wengine wakidai anatumiwa na wazungu kuhujumu nchi.
"Leo Benson Bana na wengine wachache wanahoji uzalendo wa Lissu, Bana amewahi kufanya nini cha kizalendo kwa nchi hii? Uzalendo siyo kuunga mkono serikali iliyopo madarakani uzalendo ni kupenda nchi yako" alisema John Heche
Mbali na hilo Joh Heche amesisitiza kuwa wasomi wa nchi hii wamekuwa wakilitia aibu taifa la Tanzania kutokana na maamuzi yao pamoja na kupotosha ukweli uliowazi kabisaa.
"Lissu alitoa tahadhari kwa serikali kuacha kuvunja mikataba bila kufuata utaratibu wa kisheria, serikali hii iliyotuingiza kwenye matope haya ikatoka na kusema Lissu amehongwa na wazungu kuwatetea leo mmeshindwa kesi mnatakiwa kulipa mabillion ya pesa za walipa kodi masikini kwa kuvunja mikataba bila utaratibu, Lissu kusema tena inaonekana siyo mzalendo! Hivi serikali hii inawaona Watanzania hawawezi kufikiri vizuri? na nyinyi wasomi wetu mnatia aibu sana" alisisitiza John Heche.
Katika hatua nyingine Mbungy huyo wa Tarime Vijijini John Heche amemaliza ziara yake jimboni kwake huku akiwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi, lakini pia ametoa salamu kwa baadhi ya watawala wasio waadilifu na kuwaambia hawataweza kuwazuia katika kutimiza majukumu yao.

"Vitisho vya watawala wasiokuwa waadilifu kujaribu kutuzuia kufanya majukumu yetu havitafanikiwa Asanteni Sirari kwa kujitokeza kwa wingi bila kuogopa vitisho. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu ametuwezesha kuhitimisha vizuri ziara ya majimbo yetu kuhakikisha tunasaidiana kusukuma mbele maendeleo ya watu wetu" alisema John Heche

No comments:

Post a Comment