Sunday, 6 August 2017

Chelsea vs Arsenal kutumia mfumo mpya wa penati za “ABBA” hii leo

“ABBA” ni nini? kwa sisi tunaojua mchezo wa tennis tunajua kuhusu mfumo huu wa penalty ambapo zinapigwa kwa mfumo wa AB BA AB BA badala ya ile aina ya penati iliyozoeleka siku zote ya AB AB AB AB.
Bado nimekuacha? ni hivi penati za kawaida anapiga timu moja halafu wanafuata wapinzani kisha timu iliyoanza inapiga tena lakini ABBA ni timu moja inaenda kupiga penati(A) kisha timu inayofuata inapiga mbili(BB) kisha walioanza nao wanapiga mbili (AA).
Penati hizi zilitumika katika mchezo wa nusu fainali ya wanawake u-17 kati ya Norway na Ujerumani na leo ndio zitakazoamua mshindi kati ya Arsenal na Chelsea kama timu hizo zitamaliza dakika 90 kukiwa hakujapatikana mshindi.
Chelsea wanaingia katika mchezo huu wakiwa na maingizo mapya matatu Antonio Rudiger, Timoue Bakayoko na Alvaro Morata huku Diego Costa akikosekana katika mchezo huu na Arsenal hawana shaka na Lacazette ambaye alionesha cheche katika pre season.
Alexis Sanchez anaweza kukosa mchezo huu kutokana na kutokuwa fiti 100% huku kocha Arsene Wenger amesema anahitaji ushindi tu na si kingine “wamempoteza Matic wakaleta Bakayoko na Costa wakaleta Morata lakini tunataka kile tulichifanya zidi yao katika mchezo wa FA’
Wakati Wenger akisema anataka ushindi Conte naye amesema “ni vyema tukaanza ligi kwa ushindi, Arsenal ni wagumu na wanatupa sana changamoto kwani walipotufunga kwenye FA ilikuwa mbaya kwetu lakini leo tunapaswa kuwafunga”

Huu unaweza kuwa mchezo wa kisasi kwa Chelsea kwani mara ya mwisho kukutana na Arsenal katika fainali za ngao ya hisani ilikuwa mwaka 2015 na wakapoteza kwa bao 1 kwa 0 huku fainali ya Fa msimu uliopita Cheslsea wakapigwa tena.

No comments:

Post a Comment