Tetemeko hilo lililochukua sekunde chache limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba na dakika ishirini muda ambao watu walikuwa wamelala,baada ya tetemeko kutokea baadhi yao walitafuta namna ya kuokoa maisha yao kwa kuzikimbia nyumba zao huku wengine wakiwasahau hadi watoto wadogo wao ndani ya nyumba.
Nao baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Bukoba waliozungumza na ITV wakati wakielezea juu matukio ya mara kwa mara ya tetemeko la ardhi katika Mkoa wa Kagera wameshauri watu wamrudie Mungu ili wajiepushe na matukio hayo na wameshauri pia wananchi wazingatie ushauri unaotolewa na wataalamu wa masuala ya Jiologia ili waweze kujiepusha na madhara ambayo usababishwa na tetemeko pale linapotokea.
Akizungumzia juu ya tukio hilo kwa njia ya simu Mkuu wa mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Salum Mstapha Kijuu amesema hadi sasa hakuna taarifa ya madhara yoyote yalisababishwa na tetemeko hilo na Afisa Mwandamizi wa wakala wa Jiologia tanzania,Gabriel Mbogoni aliyezungumza pia na ITV kwa njia ya simu amesema tetemeko hilo halikuwa kubwa hivyo akaendelea kuwashauri wananchi katika mkoa wa Kagera waendelee kuchukua tahadhali
No comments:
Post a Comment