Tuesday, 2 May 2017

Teknolojia mpya iliyogundulika kufanya upasuaji wa kichwa

Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Utah nchini Marekani wamevumbua teknolojia mpya ya Robot ambayo itatumika kufanya upasuaji ifikapo mwaka 2019 ambapo inategemewa kufanya upasuaji kwa haraka zaidi kuliko daktari wa kibinadamu.
Kwa mujibu wa daktari bingwa wa upasuaji William Couldwell, Robot hii ina uwezo wa kufanya upasuaji kwa usafi na ufanisi mara 50 zaidi ya binadamu wa kawaida ambapo itasaidia kuokoa vifo vinavyosababishwa na makosa ya kibinadamu kama vile kusahau vifaa vya upasuaji kwenye mwili wa mgonjwa.

Robot hii inatarajia kuanza rasmi kutumika kufanya upasuaji wa kichwa baada ya miaka miwili ijayo ambapo itaweza kugundua tatizo la mgonjwa kupitia machine ya CT Scan na inaweza kujizima iwapo itaona imesogea karibu zaidi na ubongo. Mashine hii itagharimu Dollar 100,000.

No comments:

Post a Comment