Wednesday, 10 May 2017

Rais wa Sudan Kusini amemwachisha kazi mkuu wa Jeshi Paul Malong

Taarifa kutoka mjini Jumba imeleza kwamba Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametangaza kumfuta kazi mkuu wake wa majeshi na mtu wake wa karibu Paul Malong,
Jenerali Paul Malong aliyekuwa akitajwa kama kinara wa ukabila kutoka kwenye kabila la rais Kiir la Dinka, sasa nafasi yake imechukuliwa na Jenerali James Ajongo Mawut.
Msemaji wa rais Kiir, Ateny Wek Ateny amesema kuwa hatua hii ni katika muendelezo wa mabadiliko ambayo yanafanywa na rais Kiiri na kwamba nafasi ya ukuu wa majeshi inaweza kukaliwa na mtu kwa muda wa miaka 2 hadi minne na Malong ameshika nafasi hiyo kwa muda wa miaka 3.
Mwezi Februari mwaka huu maofisa kadhaa wa juu wa jeshi walitangaza kujiuzulu nafasi zao wakimtuhumu Malong kwa kuendesha vita ya ukabila dhidi ya makabila mengine.

Inaelezwa kuwa pia Malong ndiye aliyekuwa mpangaji mkuu wa mapigano yaliyotokea mjini Juba mwezi Julai mwaka jana na kusababisha kuvunjika kwa Serikali ya kitaifa kati ya rais Kiir na mpinzani wake Riek Machar.

No comments:

Post a Comment