Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limezuiya Ziara ya Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi wa Chama Cha CUF Juliasi Mtatiro.
Mtatiro aliwasili jijini Tanga jana jioni kwa lengo la kufanya vikao vya ndani pamoja na kufungua matawi kazi ambayo ilikuwa aifanye leo na kesho.
Mwenyekiti wa CUF ,Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe amesema licha ya
kwamba hadi jana jioni walikuwa na barua kutoka jeshi la polisi ya
kuwaruhusu kuendelea na ziara ya Mtatiro lakini leo saa 3.00 asubuhi
walizuiwa.
“Tulipopewa taarifa ya kuzuiwa, tuliamua kwenda kwa OCD Tanga.
tukiambatana na mheshimiwa Mtatiro kupata maelezo ya kwa nini tuzuiwe ndipo tukaambiwa Magdalena Sakaya ametuma barua ya kuzuia mikutano hiyo kwa madai kwamba hana taarifa,”amesema Jumbe.
Mwenyekiti huyo alieleza kushangazwa kwake na kitendo cha jeshi la
polisi kufanyia kazi maelekezo ya Sakaya huku akisisitiza kwamba CUF
Tanga haimtambui kwa sababu alishafukuzwa uanachama.
“Magdalena Sakaya na Profesa Ibrahim Lipumba sisi Tanga hatuwatambui
kwa sababu si wanachama wa CUF, hao ni viongozi wa Msajili wa Vyama
vya Siasa, watambue kwamba njama zao za kuiua CUF hazitafanikiwa
kamwe,” amesema Jumbe.
Amesema Julias Mtatiro alikuwa amepangiwa kukutana na viongozi wa
kamati ya utendaji ya Wilaya ya Tanga, madiwani, wabunge, kufungua matawi
ya Kata ya Duga, Masiwani Shamba, Masiwani, Mabawa, Magaoni, Mnyanjani, Pongwe na Kwanjeka.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema
wamezuia ziara hiyo kufuatia jeshi la polisi kupokea barua mbili
tofauti zenye kupingana jambo lililoashiria kuwa kusingekuwa na amani
No comments:
Post a Comment