Wednesday, 10 May 2017

Ofisi ya Taifa ya Takwimu wametakiwa kufanya kwa bidii na weledi ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu

unnamed
   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Dkt.Chuwa amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
A
 Kaimu Mkurugenzi wa Utawala, Fedha na Masoko Bi. Lilian Karumuna wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akifafanua jambo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 A 1
 Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania tawi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (TUGHE) Bi. Raya Mikidadi akifafanua jambo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 A 2
 Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 A 3
 Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. (Picha na Veronica Kazimoto)

No comments:

Post a Comment