Sunday, 7 May 2017

Mourinho aipangia Arsenal Kikosi B


KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amewachukua wachezaji wa kikosi cha pili cha vijana, Matthew Olosunde, Demetri Mitchell na Matty Willock kwenye kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo wa ugenini dhidi ya Arsenal leo.




Mourinho alitania wiki iliyopita kwamba Arsene Wenger atafurahia kikosi atakachoteua kutokana na idadi ya mechi zinazomkabili wiki za karibuni na huku wengi wakiwa majeruhi.
Beki Mmarekani, Olosunde mwenye umri wa miaka 19, Mitchell na Willock wote miaka 20 kila mmoja, pia wamejumuishwa na Scott McTominay katika safari ya London.
Willock aliitwa pia kikosi cha kwanza cha Mashetani hao Wekundu kwa ajili ya mchezo mwngine wa Ligi Kuu dhidi ya Swansea City wikiendi iliyopita.
Mourinho hatakuwa na Marouane Fellaini, wakati Antonio Valencia pia amepumzishwa kwa mchezo wa leo Uwanja wa Emirates.




Baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Celta Vigo 1-0 usiku wa Alhamisi kwenye Nusu Fainali ya kwanza ya UEFA Europa League, bao pekee la Marcus Rashford kwa shuti la mpira wa adhabu, Mourinho alisema atawapumzisha baadhi ya wachezaji wake katika mchezo na Arsenal.



Safari ya Arsenal ni muhimu katika vita ya kuwania kuwamo ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, lakini Mreno huyo anafahamu shughuli haijakamilika katika michuano hiyo, inayotoa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao kwa timu inayotwaa taji.
Alipoulizwa kama atawapumzisha baadhi ya wachezaji Uwanja wa Emirates Jumapili kuelekea mchezo wa marudiano, alisema; "Wachezaji waliopo kundini, ni wachezaji ambao wamecheza dakika nyingi, kwa sababu tumecheza mechi tisa tangu Aprili na hii, hivyo ni mechi 10 katika wiki nne na nusu.
"Wachezaji waliopo kwenye kundi hilo, hawatacheza wikiendi ijayo," amesema.
United inaweza kuwa imetanguliza mguu moja kwenye fainali mjini Stockholm, lakini bado watalazimika kupambana katika mchezo wa marudiani dhidi ya timu ya La Liga yenye ukuta imara.

No comments:

Post a Comment