Monday, 8 May 2017

Hajji Manara:Ni kweli ajali hupangwa na Mungu 'but' nyingine zinaepukika

Msemaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Hajji Manara ametoa ushauri kwa serikali kuu imefanya mchakato wa haraka kuhakiki upya leseni za madereva ili kuepukana ama kupunguza ajali za barabarani.
Manara amesema hayo siku moja kupita tangu zilipotokea ajali mbaya zilizoweza kuua watu kadhaa katika sehemu mbili tofauti ambapo ya kwanza ilikuwa Karatu mjini Arusha iliyoweza kupoteza roho za wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 pamoja na dereva wa gari ya shule ya msingi Lucky Vicent ya Arusha, huku nyingine ikitokea jana jumapili eneo la Lusanga mkoani Tanga na kuua watu wanne na kusababisha majeruhi kadhaa.
"Ni kweli ajali hupangwa na Mungu 'but' nyingine zinaepukika....Kuna haja ya serikali kuhakiki upya leseni za udereva kama walivyohakiki vyeti vya magumashi". Alisema Manara kupitia ukurasa wake wa instagramu
Katika hatua nyingine, Miili ya marehemu waliopata ajali ya Arusha wanaagwa leo katika uwanja wa Amri Abeid mkoani humo.

Kutokana na msiba huo kugusa taifa kiujumla hivyo kusababisha Bunge kwa ujumla limeweza kuchangia kiasi cha Milioni 100 kama rambi, milioni 86 zimetokana na michango ya wabunge wenyewe katika kikao cha leo ambapo waliamua posho zao wazielekezee kwa wafiwa wote waliopoteza watoto,ndugu zao katika ajali hiyo hiyo ya Arusha huku Bunge lenyewe limetoa milioni 14 ambazo kwa ujumla zimefikia milioni 100.

No comments:

Post a Comment