Maelfu ya wanaomuunga mkono Macron walisherehekea katika kati mwa Paris wakipeperusha bendera.
Akiwa na miaka 39, Macron anakuwa rais waumri mdogo zaidi wa kuchaguliwa kuwahi kuiongoza Ufaransa na wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya vyama viwili vikubwa vya siasa nchini humo.
Katika taarifa yake, amesema kwamba Ufaransa imefanikiwa kufungua ukurasa mpya katika historia yake na kwamba alikuwa na ndoto ya kuwa mpiga mbiu wa nchi hiyo kwa kugunduliwa upya kwa matumaini na imani.Mshndi huyo wa nafasi ya urais ametoa hotuba yale ya kwanza akiwa ni raisi mteule.
"Wafaransa wenzangu, mlioko ndani na nje ya ufaransa, baada ya vita ya muda mrefu vya kidemokrasia, na kuchagua kuweka imani yenu juu yangu. Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima kubwa," amesema.
Macron anasema ni heshima kubwa na mmenipa wajibu mkubwa wa kutekeleza, bila kauli yoyote kwangu, natoa shukrani zangu za dhati kutoka ndani ya moyo wangu.
"Shukrani hizi zimfikie kila mmoja wenu, kwa kura yako na kuniunga mkono. Sitasahau kamwe, nitakuwa muangalifu sana na nitahakikisha kwa nguvu zangu zote naheshimu imani yenu kwangu."
No comments:
Post a Comment