Thursday, 1 September 2016

Wakuu wa mikoa ya Mbeya na Songwe waongoza wananchi katika tukio la kupatwa kwa jua

01
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mh. Chiku Galawa wakiangalia kupatwa kwa jua kwa miwani maalum katika eneo la Tazara Relini Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambapo wageni na wananchi kutoka maeneo mbalimbali na mikoa ya jirani wakiwemo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka ulaya wamekuja kushuhudia tukio hilo linalotokea kwa nadra.
1
Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii TTB Bw. Geofrey Meena akiangalia tukio la kupatwa kwa jua kwa miwani maalum wakati wa kushuhudia tukio hilo katika eneo la Taraza Relini Rujewa wilayani Mbarali.
2
Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena kulia pamoja na pamoja na wafanyakazi wenzake wa TTB kutoka kulia Gladstone MlayMkuu wa Utalii Kanda ya Ziwa , Irene MvileAfisa Utalii Habari na ErnestMususa Mhasibu wakishuhudia tukio hilo kwa pamoja.
  6
Mkuu wa Mawasiliano TTB eofrey Tengeneza akizungumza na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika eneo hilo ili kushuhudia tukio hilo.
7
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala  akiwa pamoja na viongozi wa mkoa huo Katikati Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw William Ntinika na Mbunge wa jimbo la Mbarali.
8
Mkuu wa mkoa wa Songwe Mh. Chiku Galawa akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa Mstaafu Bw.Eraston Mbwilo.

9
Baadhi ya wanafunzi wakishuhudia tukio hilo.
10 11
Mwananchi wa Rujewa Kennedy Lutambi akishuhudia tukio hilo.
13
Mwandishi wa Gazeti la Uhuru Issa Mohammed naye hakuwa nyuma kushuhudia tukio hilo adimu.
5
Hivi ndivya hali ilivyokuwa baada ya juwa kupatwa matukio tofauti yakionyesha lilipokuwa likipatwa na kuachiwa.
14 15 16 18

No comments:

Post a Comment