Thursday, 1 September 2016

Usajili wavigharimu shilingi tril 3.3, vilabu EPL

Vilabu vya Ligi Kuu ya England vimetumia jumla ya pauni bilioni 1.165 ( trillion 3.3 za Kitanzania) kwa ajili ya usajili katika dirisha la usajili lililofungwa usiku wa kuamkia leo.
Katika siku yake ya mwisho, jumla ya pauni milioni 155 zimetumika kwa ajili ya usajili, na kuipiku rekodi ya mwaka 2013 ambapo katika siku ya mwisho, zilituika pauni milioni 140 pekee.

Pesa zilizotumika msimu huu £1.165bn zimeipiga kikumbo rekodi ya msimu uliopita ambapo usajili ulivigharimu vilabu kiasi cha pauni milioni 870 pekee.
Wastani wa matumizi kwa mchezaji mmoja msimu huu ni pauni milioni 60, ambapo mchezaji aliyesajliwa na gharama kubwa zaidi ni Paul Pogba aliyesajiliwa Man United kwa dau la pauni milioni 89.
Jumla ya vilabu 13 vimevunja rekodi zao zenyewe kwa kuongeza pesa za usajili huku vilabu vyote pia kwa mara ya kwanza vikinufaika pauni bilioni 5.1 zinzotokana na mkataba wa matangazo ya televisheni.

Klabu mbili za Manchester, City na United kwa pamoja zimetumia zaidi ya pauni milioni 150 ambapo meneja mpya wa Manchester United, Jose Mourinho, alimnunua Paul Pogba kwa rekodi ya dunia.

Pia amemnunua kiungo wa kati kutoka Armenia Henrikh Mkhitaryan na beki wa Ivory Coast Eric Bailly, ambao kwa pamoja wamegharimu pauni milioni 30.

City, chini ya Pep Guardiola, imemnunua kiungo wa kati Leroy Sane kutoka Schalke kwa £37m kisha wakalipa Everton £47.5m kumchukua beki John Stones.

Antonio Conte wa Chelsea ametumia pauni milioni 120, ikiwemo £34m kumrejesha beki Mbrazil David Luiz kutoka Paris St-Germain na £33m kumpata mshambuliaji Mbelgiji Michy Batshuayi kutoka Marseille.



No comments:

Post a Comment