Thursday, 1 September 2016

Tanzania yateuliwa kuwa mwenyekiti wa asasi ya siasa, ulinzi SADC

Makamu wa Rais Samia Suluhu 
Swaziland. Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali  umemalizika leo   mjini Mbabane Swaziland ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi muhimu na nyeti ya Siasa, Ulinzi na USalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC- (SADC Organ On Politisc, Defence and Security Cooperation).
Katika mkutano huo, ambao Makamu wa Rais Samia Suluhu alimwakilisha Rais John Magufuli, Angola imeteuliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa asasi hiyo.

Jukumu kubwa la asasi hiyo litakuwa ni kuangalia masuala yote yanahusiana na Siasa, ulinzi na usalama katika ukanda wa SADC huku changamoto kubwa ikiwa ni namna ya kutafuta suluhu ya kudumu hususani katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC na Lesotho.

Akizungumzia mambo muhimu yaliyojiri kwenye Mkutano huo wa 36 wa SADC mjini Mbabane - Swaziland, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa na amehimiza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Makamu wa Rais amesema kuwa nchi wanachama wa SADC kwa sasa wanatakiwa kuongeza juhudi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi haraka kama hatua ya kujenga ustawi bora wa wananchi wa kanda hiyo.

No comments:

Post a Comment