Na Daudi Manongi,MAELEZO
Shirika la Maji Safi na Maji taka
Dar es Salaam (DAWASCO) limetangaza kuzima mtambo wa kuzalisha Maji wa
Ruvu Juu kwa wakazi wa Dar es salaam na Mji wa Kibaha Pwani kwa saa 14
kesho Ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tano usiku.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa
kwa vyombo vya Habari na ofisi ya mahusiano ya shirika hilo leo jijini
Dar es Salaam inaeleza kuwa sababu kuu ya kuzimwa kwa mtambo huo ni
kuruhusu usafishaji wa bomba jipya na kufanya majaribio ya sehemu ya
mtambo mpya wa Maji wa Ruvu juu.
Pia zoezi hili linahashiria hatua
za mwisho za mtambo huo kukamilika na kuanza kutumika ili kuondoa tatizo
la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo
huo.
Maeneo ambayo yatakosa maji ni
Mlandizi Mjini , Ruvu darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga,
Janga, Mbagala, Visiga, Lulinzi, Kibamba, Kibamba njia panda, Shule
kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba hospital, Kwa mkinga, Luguruni
,Maili 35, Zogowale, Misugusu,Tanita, Kibondeni, Kwa mathias, Nyumbu,
Msangani, Kwa mbonde, Picha ya Ndege, Sofu na Gogoni.
Pia zoezi hili linahashiria hatua
za mwisho za mtambo huo kukamilika na kuanza kutumika ili kuondoa tatizo
la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo
huo.
Aidha Shirika linatoa ushauri kwa wananchi kuhifadhi maji na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.
No comments:
Post a Comment