Monday, 5 September 2016

Shamsa Ford atoboa siri kupata 'mume'

Msanii wa filamu nchini, Shamsa Ford akiwa na mumewe Chidi Mapenzi.

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford ambaye amefunga ndoa na mfanyabishara Chidi Mapenzi wiki iliyopita amefunguka na kutoa chanzo cha yeye kukutana na mpenzi wake huyo ambaye amefunga naye ndoa na kusema chanzo kilikuwa ni chakula.
Shamsa ford anasema kuwa siri ya mahusiano aijuae ni Mungu kwani yeye alikuwa anapita karibu kila siku kwenye duka la nguo la Chidi Mapenzi tena bila hata kusalimia kumbe huyo mtu ambaye anampita kila siku ndiye mume aliyeandaliwa na Mungu.

"Kiukweli siri ya mahusiano aijuae ni Mungu. Nilikuwa napita tu ofisini kwako tena bila hata salamu, nakumbuka siku niliyokuwa nakula karibu na ofisi yako kwa bahati mbaya chakula kilinimwagikia kwenye nguo na ikanibidi niingie ofisini kwako ili niweze kununua nguo mpya. Daa kumbe Mungu alikuwa ananikutanisha na mume wangu kipenzi jamani. Asante Mungu kwa mume bora uliyenipa. Muda wa Mungu ndiyo muda sahihi"alisema Shamsa Ford

No comments:

Post a Comment