Monday, 5 September 2016

Mkusanyiko wa barabara hatari zaidi Afrika

Roho mkononi ukiamua kupitia hapa kwa gari!
  Kuna barabara katika mataifa ya Afrika ambazo hazipitiki. Utadhani ni njia shambani. Hizi hapa picha za barabara zilizo katika hali ya kutamausha.


 Ni wazi wahandisi walisahau kuweka daraja.  Lazima uwe dereva mwenye ujasiri na ushupavu wa aina yake ili kupitia hapa.

Ni kama wajenzi wameenda kula na wananuia kurudi baadaye….hii barabara kamwe haijakamilika!

 Gari la 4×4 lina uwezo wa kupenya katika barabara mbovu, lakini hapa helikopta ingefaa zaidi!
 Hata malori hayawezi kupitia kwenye kidimbwi cha matope.

Kwani wachimba madini walisahau kuziba mashimo?

 Tope zaidi.
 Kizuizi tosha kwa madereva watundu wa malori walio na mazoea ya kupakia mizigo juu kupita kiasi. Na je, hiyo ni stegi ya basi?
 Hapa tope tu!
 Wanasayansi wa akiolojia hawatahitaji kutoa kijasho hapa kufanya utafiti wao wa mambo ya kale.
 Barabara hizi zinahitaji ujasiri, ushupavu na uvumilivu wa ajabu ili kupitia. Zingine si mbovu tu lakini pia ni hatari kwa maisha!

No comments:

Post a Comment