Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata tiketi ya mabasi ya Mradi wa
Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo hicho
kuelekea Posta. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,
Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga naye akiwa mmoja wa wasafiri wa mabasi
hayo. Masauni aliyapanda basi la Mwendo kasi mara baada ya kufanya ziara
ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu
pamoja na usalama wa abiria. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiigusisha tiketi yake katika mashine ya
Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini
Dar es Salaam ili mruhusu kuingia ndani ya stendi hiyo kwa ajili ya
kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo hicho kuelekea Posta. Mara
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo
kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiingia ndani ya Basi la Mradi wa Mabasi
ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kusafiri na basi hilo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua
mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa
mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam akitoka kituo cha
Ubungo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na
usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitelemka katika moja ya mabasi ya mradi
wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam katika kituo
cha Nyerere, Posta. Masauni alipanda basi hilo akitokea Ubungo baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua
mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiondoka katika Kituo cha Mabasi ya
Mwendokasi cha Nyerere, Posta, mara baada ya kusafiri na usafiri huo
akitokea Ubungo, jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu
pamoja na usalama wa abiria. Katikati ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Felix Mwagara, MOHA
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameupongeza Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi
ya UDA-RT wa jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi waendelee
kuyatumia mabasi hayo wanaposafiri sehemu mbalimbali jijini humo.
Mhandisi Masauni ameyasema hayo
jana mara baada ya kusafiri na mabasi hayo kutoka kituo cha mabasi hayo
cha Ubungo mpaka katikati ya jiji kwa lengo la kujionea jinsi mabasi
hayo ya mwendokasi yanavyohudumia abiria pamoja na kuwapa moyo wananchi
kuwa usafiri huo unatumiwa na mwananchi wa aina yeyote.
Akizungumzia usafiri huo, Masauni
alisema mradi huo umerahisisha sana usafiri kwani ametumia dakika chake
akitokea Ubungo hadi Posta katikati ya jiji bila usumbufu wowote, hivyo
mradi huo ameomba uendelee kulindwa pamoja na kutunzwa na UDA-RT na
wananchi wenyewe kwa ujumla.
“Mimi kwa kweli nimeufurahia sana
usafiri huu, Serikali imefanya jambo kubwa sana kwa wananchi wake, kwa
kuwajali wananchi kwa kuuleta mradi huu ambao unarahisisha safari kwa
uharaka zaidi na pia unapendezesha jiji kwa jinsi magari yalivyo
nadhifu,” alisema Masauni ambaye pia alilipa nauli kwa kupanga foleni
kama wananchi wengine wanavyofanya wanapotaka kusafiri na usafiri huo.
Masauni aliongeza kuwa;
“Nimefarijika sana na lugha ya adabu na tulivu ambayo wanaitumia
madereva wa mabasi hayo wanapowatangazia wananchi vituo mbalimbali vya
kushuka na kuingia kwenye mabasi hayo, hii inasaidia kuwa na mawasiliano
mazuri na abiria, pia inaonesha madereva hao wamefunzwa vizuri na
wanaipenda kazi yao.”
Hata hivyo, Masauni alitoa
ushauri kwa uongozi wa mabasi hayo, kuruhusu wananchi waingie ndani ya
mabasi hayo kwa idadi ambayo haitaleta kero kwa abiria wengine ili
kupunguza wingi wa abiria hao kwa lengo la kuepuka mbanano mkubwa wa
abiria.
Pia aliwataka wananchi wa jiji
hilo kuyatunza mabasi hayo, na pia kukubali maelekezo ya madereva
wanapotoa matangazo wanapokuwa safarini kuelekea maeneo mbalimbali ya
jiji.
Naibu Waziri huyo alipanda mabasi
hayo akitokea Ubungo mara baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza
kwa kutembelea Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kwa lengo la kukagua mabasi
mabovu pamoja na usalama wa abiria wanaosafiri na mabasi hayo. Masauni
pia alifanya ziara hiyo ya ghafla kwa kutembelea Stendi ya Kibaha,
mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment