Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akitembelea
eneo la kijiji cha Ntare kata ya Itera wilayani Kyerwa kujionea ukame
unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ulivyoathari mazao ya ndizi na
kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera na kuwaomba wananchi wa mkoa huo
wabadilike waanze kulima mazao mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda
mfupi.
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista akiwa ziarani wilaya ya
Kyerwa na kujionea mazo la viazi ambalo pia linaweza kulimwa wilayani
humo.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Kyerwa, Kagera).
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Kyerwa, Kagera
Ukame unaotokana na mabadiliko ya
tabia nchi ulioathari mazao ya ndizi na kahawa wilaya Kyerwa mkoani
Kagera umemlazimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama kuwaomba wananchi wa mkoa huo
wabadilike waanze kulima mazao mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda
mfupi.
Athari hiyo ya ukame imemlazimu
Waziri Mhagama kuwataka wananchi wa wilaya hiyo na mkoa wa Kagera kwa
ujumla w0aanze kulima mazao mengine yanayokomaa kwa muda mfupi yaweze
kuwapunguzia adha ya upungufu wa chakula unaotokana na kutegemea zao la
ndizi pekee.
Akiwa katika kijiji cha Ntare
kata ya Itera wilayani Kyerwa Waziri Mhagama aliongea na wananchi wa
kata hiyo ambapo alisema “Mabadiliko ya tabia nchi ni makubwa,
msiendelee kutegemea zao moja tu la chakula la ndizi, ni lazima mkubali
sasa tuende kwenye mazao mengine ya chakula, limeni mihogo, limeni
mahindi. Nendeni kwenye mazao yanayokomaa kwa muda mfupi, vinginevyo
tukisema kila kila mwaka tuendelee kutegemea kahawa na ndizi kwa hali ya
hewa ilivyo sasa tutaendelea kukosa chakula”.
Waziri Mhagama aliyataja mazao
hayo kuwa yanaweza kukomaa kwa muda mfupi kuanzia miezi mitatu ndiyo
yanaweza kuwa mkombozi wa katika kukabiliana na upungufu wa chakula na
kuwahakikishia wananchi chakula cha kutosha hatua ambayo itawafanya
waendelee na shughuli zenye tija kwa maendeleo yao.
Mkulima wa kata hiyo Shakiru Issa
anathibitisha kuwa upo uwezekano wa kulima mazao mengine zaidi ya ndizi
na kahawa ambayo yanamuongezea kipato ambapo yeye analima pia zao la
viazi mviringo kwa ajili ya chakula pamoja na kuuza hatua inayomsaidia
kumuongezea kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.
Ili kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi Waziri Mhagama amewataka wananchi wa mkoa wa Kagera kuacha
tabia ya kuchoma mapori moto mara moja kwa kuwa tabia hiyo huhatarisha
maisha ya watu, kupoteza mazao shambani,miti na hifadhi ya misitu ambayo
ndiyo kivutio kikuu cha mvua.
Aidha, ziara hiyo wa Waziri
Mhagama imekuwa faraja kwa wananchi wa Kata ya Itera ambapo amemwagiza
Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia
Jenerali Mbazi Msuya aende kufanya tahmini ya hali ukame ilivyo athiri
wilaya hiyo na kutoa taarifa mapema iwezekanavyo.
Katika kuhakikisha upatikanaji wa
chakula cha kutosha wilayani Kyerwa, Waziri Mhagama ametoa wito na
kumuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Mstaafu Shaban Lissu pamoja kulima
zao la ndizi, aanza haraka kampeni ya kuwahamasisha wananchi hao kulima
mazao yanayokomaa kwa muda mfupi ambayo yataweza kuwapatia chakula cha
kutosha kwa mahitaji yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment