Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe
Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Wakuu wa
Shule za sekondari Wilayani humo
Na Mathias Canal, Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe
Deogratius Ndejembi amewaagiza wakuu wa shule za Sekondari zote za
Wilaya hiyo kuhakikisha wanafikia ufaulu kuanzia asilimia 41% ili
kuakisi hali ya ukuaji wa ufaulu nchini na kupata wanafunzi waliopikwa
vyema darasani ili kuwa na wasomi wenye weledi pasina mashaka.
Dc
Ndejembi amesema kuwa hatarajii kusikia shule mojawapo Wilayani humo
ikiwa imeshika mkia Kiwilaya, Mkoa ana Taifa kwani kufanya hivyo ni
kuonyesha jinsi ambavyo walimu hawakujiandaa vyema katika kuwaimarisha
wanafunzi darasani ili kufikia ufaulu mahususi na kulijenga Taifa letu
katika misingi bora ya elimu.
Ndejembi alisema kuwa anataraji kushirikiana na Afisa elimu sekondari ili kutoa hamasa kwa shule ambazo
zitafanya vyema katika mitihani yao ili kuamsha ari kwa shule zingine Wilayani humo. Walimu hao wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea, kuwa na hofu ya Mungu, na kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa katika kufundisha wanafunzi kwani walimu wana wajibu mkubwa wa kuwafanya wanafunzi kufaulu katika mitihani yao.

Sambamba na hayo pia Dc Ndejembi amewataka walimu hao kutokuwa na madaraja kati yao na wanafunzi
wao kwani kufanya hivyo ni kutengeneza chuki kutoka kwa wanafunzi kwenda kwa walimu ambapo pia inapelekea kuyachukia masomo yanayofundishwa na walimu hao.
wao kwani kufanya hivyo ni kutengeneza chuki kutoka kwa wanafunzi kwenda kwa walimu ambapo pia inapelekea kuyachukia masomo yanayofundishwa na walimu hao.
No comments:
Post a Comment