Kocha wa Yanga, Hans Pluijm alisema winga huyo hana nafasi katika kikosi chake lakini taarifa za ndani zinasema kamati imepanga kukutana kujadiliana juu ya uwezekano wa kumrejesha kundini.
Nyota huyo aliyeondoka Yanga mwaka 2015 kuelekea Free States ya Afrika Kusini, hivi karibuni alivunja mkataba na klabu hiyo na sasa yupo jijini Dar.
Inasemekana Ngassa alilazimika kusitisha mkataba na klabu hiyo ya Afrika Kusini, lakini taarifa za kuaminika kutoka Yanga, kabla ya kufikia hatua hiyo aliwaomba kutaka kumalizia soka lake Jangwani.
Lakini Kocha wa City, Kinnah Phiri ambaye ndiye alimsainisha Free States baada ya msimu wa 2014/15, alisema kuwa yupo tayari kumpa mkataba hata leo kwani anamjua sana.
Hata hivyo, Mlawi huyo ameeleza hofu yake kuwa anaweza kumkosa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kumlipa mshahara.
“Hata kama ni leo akinihakikishia yupo tayari kucheza Mbeya City, nawaagiza viongozi kumpa mkataba. Unajua mchezaji huru anaweza kujiunga na timu muda wowote hata kama usajili ukiwa umekwisha.
"Ngassa ni mchezaji aliyekamilika na ndiyo maana nilifanya juu chini asajiliwe Free States, japo sijajua ni nini kilitokea mpaka kufikia hatua ya kukatisha mkataba,” alisema Phiri.
No comments:
Post a Comment