Katibu
wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO
SHAIBU akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi
ya kumpokea kiongozi yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE
ambaye naye amekumbwa na timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo
yatafanyika Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili
Na Mwamvita Mtanda
Katibu wa Itikadi mawasiliano na
uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO SHAIBU akizngumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi ya kumpokea kiongozi
yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE ambaye naye amekumbwa na
timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo yatafanyika Jijini Dar es salaam
siku ya Jumapili
Story ambayo bado ipo maskioni
mwa watanzania walio wengi ni mwenendo wa bunge la Jamhuri ya muungano
wa Tanzania na mizengwe yake ambayo imesababisha wabunge saba wa vyama
vya upinzani kusimamiswa kushiriki shughuli za bunge kwa vipindi Tofauti
tofauti akiwemo mbunge kutoka ndani ya chama cha Act wazalendo Mh ZITTO
ZUBERI KABWE na wabunge wa vyama vya UKAWA.
Sakata hilo limeendelea kuchukua
Headline katika maeneo mbalimbali ambapo asubuhi hii chama cha ACT
wazalendo kupitia kwa kiongozi wao ADO SHAIBU wamejitokeza mbele ya
wanahabari kueleza msimamo wa chama chao kuhusu sakata hilo.
Akizungumza na wanahabari leo
Katibu huyo wa itikadi mawasiliano na uenezi wa ACT ADO SHAIBU ameeleza
kuwa chama hicho kimeandaa mapokezi ya kiongozi wao ambaye amekumbwa na
adhabu hiyo mapokezi ambayo yanataraji kufanyika Jijini Dar es salaam na
baadae kufwatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara ambao umepangwa kufanyika
katika viwanja vya ZAKIEM mbagala lengo likiwa ni kuwapa nafasi wabunge
hao kueleza ukweli wa yale yanayoendelea bungeni Dodoma.
Pamoja na mandalizi hayo chama
hicho kimewaandikia barua makatibu wa vyama vya upinzani ambao nao
wanapinga adhabu hiyo kutoka CHADEMA,CUF,na NCCR-MAGEUZI kuwaomba
kuungana nao katika mapokezi hayo ambayo yamepewa jina la OPERATION
LINDA DEMOCRASIA na bado hawajapata majibu yao lakini wanaamini
wataungana nao katika Operation iyo ambayo itafwatiwa na mikoa mingine
takribani minne.
No comments:
Post a Comment