
Mwanamuziki wa kufoka kutoka
Marekani 50Cent alilazimika kulipa faini ya dola elfu ishirini pesa za
Marekani baada ya kutumia maneno yenye matusi alipokuwa akiwatumbuiza
mashabiki wake huko katika kisiwa cha St Kitts and Nevis.
Fifty
cent ambaye anafahamika kwa jina kamili Curtis Jackson alikuwa
amepangiwa kuwa 'Mcee' katika tamasha hilo la muziki huko Caribbean
lakini alipopanda jukwaani mashabiki walimsihi awape kionjo cha muziki
wake.
50 cent hakufahamu alikuwa amevunja sheria hadi alipofika katika uwanja wa ndege siku ya Jumapili akikusudia kuondoka.
Hata hivyo maafisa wa forodhani walimkamata na kumzuilia hadi jumatatu alipofikishwa mbele ya hakimu na kusomewa mashtaka yake.

No comments:
Post a Comment