Kaimu
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Bw. Paul Rwegasha akimuonyesha uchafu zaidi Meneja Rasilimali
Watu Mafunzo, Bw. Abdul Mkwizu (kushoto), wakati wakifanya usafi eneo la
Kigilagila Relini, ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira
Duniani, Juni 5, 2016
Mkuu
wa Kitengo cha Mazingira cha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA) Bw. Jofta Tuimanywa (aliyenyoosha mkono), akisisitiza jambo kwa
wafanyakazi wenzake, wakati wakifanya usafi kwa kushirikiana na wakazi
wa mitaa ya Kigilagila Relini na Vituka kwenye eneo la nyuma ya uzio wa
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Juni 5, 2016
ni Siku ya Mazingira
Dunia.
Wakazi
wa Mitaa ya Kigilagila Relini na Vituka wakiwa pembeni ya kibao
kinachokataza utupaji wa taka, katika eneo la nyuma ya Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mara baada ya kumaliza kufanya
usafi. Juni 5 ni Siku ya Mazingira Duniani.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Laurent Mwigune (mwenye suti) jana akishiriki zoezi la
kufanya usafi maeneo mtaa wa Kigilagila Relini, ikiwa ni muendelezo wa
zoezi la usafi kuelekea Siku ya Mazingira Duniani, Juni 5, 20916.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Bw. Paul Rwegasha (mbele anayetzama kamera), akizungumza na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), na Wakazi wa
Mitaa ya Kigilagila Relini na Vituka, mara baada ya kumaliza kufanya
usafi nyuma ya ukuta wa JNIA, ikiwa ni muendelezo wa kuelekea
maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, Juni 5, 2016.
Wafanyakazi
wa TAA kuanzia kushoto Mwanaisha Athuman, Asha Lusehere na Magareth
Mushi , wakishirikiana na wakazi wa Mtaa wa Kigilagila Relini kufanya
usafi wa mazingira nyuma ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere. Juni 5 ni kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.
Wafanyakazi
wa TAA kuanzia kushoto Mwanaisha Athuman, Asha Lusehere na Magareth
Mushi , wakishirikiana na wakazi wa Mtaa wa Kigilagila Relini kufanya
usafi wa mazingira nyuma ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere. Juni 5 ni kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.
Antony
Kipobota wa TAA (katikati mwenye shati la mistari) akishirikiana na
wafanyakzi wenzake kuzoa taka ikiwa ni mwendelezo wa kuelekea
maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, Juni 5, 2016. Kaulimbiu
Kitaifa ni Tuhifadhi vyanzo vya Maji kwa uhai wa Taifa letu.
No comments:
Post a Comment