Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
Serikali
kufanya marekebisho ya Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kieletroniki
ili kuwezesha watanzania kumiliki hisa zitakazouzwa na Kampuni za
Mawasiliano kupitia soko la hisa.
Hayo
yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (Pichani)alipokuwa akiwasilisha Bungeni muswada wa
Sheria ya Fedha ya mwaka 2016.
“Mhe.
Naibu Spika, sehemu ya nne inapendekeza marekebisho katika sheria ya
Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, sura 306 kama ifuatavyo, kufuta
kifungu cha 6(2d) na kukiandika upya ili kuweka sharti kwa kampuni za
mawasiliano kuwasilisha Katiba ya Kampuni itakayothibitisha muundo wa
umiliki wa hisa kama mojawapo ya taarifa zinazopaswa kuwasilishwa wakati
wakuomba leseni,” alifafanua Mhe. Mpango.
Aidha
Mhe. Mpango aliendelea kwa kusema kwamba, watoa huduma za Mawasiliano
ya Kielektroniki watawekewa sharti la kuuza hisa zao kwa Umma na
kusajili hisa zao katika soko la hisa Nchini Tanzania ili kutoa fursa
kwa watanzaniai kununua hisa na kumiliki asilimia 25 ya Kampuni hizo.
Kutokana
na marekebisho ya sheria hiyo, kampuni za huduma za Mawasiliano ya
kielektroniki ambazo tayari zimesajiliwa hapa Nchini zitawajibika
kujioredhesha katika soko la hisa na kuuza hisa zao ndani ya kipindi cha
miezi sita kuanzia Julai 01, 2016.
Vile
vile kampuni ambazo zitasajiliwa baada ya Julai 01, 2016 zitawajibika
kuuza hisa zao na kujioredheshsha katika soko la hisa ndani ya kipindi
cha Miaka miwili kuanzia Julai 01, 2016.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe.
Hawa Ghasia amesema kwamba kamati imekubaliana na marekebisho hayo aidha
kamati inaishauri Serikali kuweka tafsiri ya watanzania ili kuwezesha
hisa hizo kuuzwa kwa watanzania pekee na pia kuangalia suala la miezi
sita kwa makampuni yaliyosajiliwa lisilete utata kwenye utekelezaji
wake.
No comments:
Post a Comment