Refa mmoja raia wa Sweden, alimpa
kwa mpigo kadi mbili za njano mwanasoka Adam Lindin ljung-kvist, akiwa
uwanjani, kwa kosa la kutoa hewa mbaya.
Mchezaji huyo alipokuwa
katika harakati za kushangaa kuhusiana na hatua ya refa huyo, alipigwa
kadi nyekundu na kuondolewa uwanjani.Refa huyo ametaja kitendo cha Adam cha kutoa ushuzi , kama tabia isiyo ya mchezaji.
Lakini kulingana na Adam, alidhani alikuwa akifanya hivyo kimaumbile tu na wala hakuwa na nia ya kumchafulia refa hewa.
Taarifa hiyo imeibua malumbano makubwa kote duniani katika mtandao wa kijamii, huku wengine wakisema kuwa hiyo ni mara ya kwanza kwa mchezaji soka kupigwa kadi nyekundu kwa sababu ya kuchafua hewa.
Amesema kuwa ameshangazwa sana na refa kumtimua, huku akiongeza kuwa, kocha na wachezaji wenzake hawakuamini walipomuona akirejea katika eneo la wachezaji wa ziada na kuwaambia kuwa amepigwa kadi nyekundi kwa "kushuta."
Adam, mwenye umri wa miaka 25 anaichezea timu ya Pershagen SK, inayo burura mkia katika ligi kuu nchini Sweden.
No comments:
Post a Comment