Mataifa 6 waanzilishi wa Muungano wa
Ulaya EU wanakutana leo kujadili mustakabali wao wa baadaye baada ya
Uingereza kuamua kujiondoa kutoka kwa muungano huo.
Mawaziri wa
mambo ya nje wa Ujerumani, ufaransa,Italy, Ubelgiji, Luxembourg na
Uholanzi wanatarajiwa kuanzisha mchakato huo pasi na kuwa na ngoja
ngoja.Tayari rais wa tume ya muungano wa Ulaya , Jean-Claude Juncker, amesema anataka kuanzisha majadiliano mara moja ya jinsi Uingereza itakavyotoka rasmi kutoka EU .
Bw.Juncker amesema haieleweki kwamba swala hilo likumbwe na hadi waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ang'atuke kutoka madarakani baada ya kushindwa katika kura hiyo ya maoni iliyoamua nchi hiyo ijibandue kutoka Umoja wa Ulaya.
Mawaziri hao pia wanatarajiwa kuweka masharti mapya yatakayowazuia wanachama wengine kuiga mfano wa Uingereza,baada ya vyama vya mrengo wa kulia katika mataifa mengi duniani kupongeza uamuzi huo wa Uingereza kujitoa kutoka muungano wa Ulaya...
Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, amewatahadharisha wenzake kutokuwa na hamaki na kutaka kuchua hatua za kama kuilipizia kisasi Uingereza .
Ameomba kuwepo kwa subra na umakini katika kulishughulikia swala hilo ambalo anasema linapaswa kuongozwa tu na vipi kushughulikia mahitaji ya raia wa jumuiya ya muungano wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment