Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amewaonya
wanasiasa wanaomchelewesha kufanya kazi ya kuwatumikia Watanzania.
Rais
Magufuli ameyasema hayo muda mfupi uliopita baada ya kupokea ripoti ya
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Amesema
haiwezekani uchaguzi umepita na mshindi amepatikana lakini wanasiasa
hao wanaendeleza siasa ilhali wananchi wanataka watumikiwe wapate
maendeleo.
Rais
amesema hatawavumilia viongozi wa siasa wenye lengo baya na nchi na
kuwataka waweke maslahi ya Taifa mbele badala ya vyama vyao.
Amewataka kufanya siasa baada ya miaka mitano ambapo wananchi watawapima kile walichokifanya kwa muda wote huo.
Awali
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva
alisema suala la Kura ya Maoni halikusitishwa kama baadhi ya watu
wanavyosema bali iliahirishwa kwa kuwa wakati kura hiyo ilipotakiwa
kupigwa Aprili Mwaka jana, Tume ilikuwa na jukumu kubwa la kuandaa
uchaguzi Mkuu.
Kutokana
na hali hiyo, Jaji Lubuva alisema Tume haikuwa na uwezo wa kubeba mambo
mawili makubwa kwa wakati mmoja. Jaji Lubuva amesema kutokana na zoezi
la Uchaguzi Mkuu kumalizika rasmi, Tume iko tayari kuanza mchakato wa
kura ya maoni.
Kuhusu
suala hilo la Kura ya Maoni, Rais Dk Magufuli amemhakikishia Jaji
Lubuva kuwa serikali italiamualia mara baada ya Tume kulifikisha
serikalni.
No comments:
Post a Comment