Kibarua cha Paris Saint-Germain (PSG) kimeota nyasi
Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) imetangaza kuwa imeachana na
aliyekuwa kocha wake, Laurent Blanc ambaye amedumu klabuni hapo katika
nafasi hiyo kwa miaka mitatu.
Kuondoka kwa Blac, beki wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa
ya Ufaransa, kunampa nafasi kocha wa zamani wa Sevilla, Unai Emery
ambaye ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi hiyo.
Blanc aliteuliwa kuwa kocha wa PSG mwaka 2013 na kuingozia timu hiyo
kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligue 1, makombe mawili ya Coupe de
France na ubingwa mara tatu wa kombe la Coupe de la Ligue.
Kuondoka kwake kunakuja baada ya Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi
kunukuliwa akitoa kauli wiki chache zilizopita kuwa kutakuwa na mchakato
wa kukijenga upya kikosi cha timu yao .
Blanc ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia
timu hiyo, Februari mwaka huu, anatarajiwa kulipwa euro milioni 22 ikiwa
ni fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wake.
Kuondoka kwa Blac kumekuja ikiwa ni siku chache pia tangu klabu hiyo
ilipomruhusu mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ambaye amemaliza mkataba
wake.
No comments:
Post a Comment