Tuesday, 28 June 2016

Wananchi wanaoishi kandokando ya reli kuondolewa kinguvu

  Na Chrispino Mpinge
 
Wizi wa miundombinu, uchakavu wa reli pamoja na shuguli za kibinadamu zimeonekana kuwa chanzo kikuu cha ajali za Treni hasa katika maeneo mengi ya njia hizo hali inayosababsha hasara kwa serikali ya mabilioni ya fedha kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa reli hizo.


Changamoto hiyo imetolewa na mkuu wa usalama wa reli nchini Mhandsi Faustin Kataraia mjini Morogoro wakati wa kikao cha kazi kilichoshirikisha wakuu wa vitengo vya usafirishaji wa reli mkoani Morogoro ambapo ajali za Treni kutokea mara kwa mara imekuwa changamoto inayodidimiza usafiri huo hali inayosababisha serikali kukosa mapato.

Kufuatia kauli ya mkuu wa usalama wa reli mkuu wa mkoa wa Morogoro ameagiza mamlaka hiyo kuandaa utaratibu wa kuwapa elimu wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za kilimo kando ya reli na kufikia mwezi Agosti mwaka huu waondoke na kuacha wazi maeneo hayo ili kuepusha uharibifu wa miundombinu hiyo.

No comments:

Post a Comment