Na Eliphace Marwa-Maelezo
Benki
ya Dunia imeahidi kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania kifedha ili
iweze kutekeleza majukumu yake ya utoaji wa huduma za msingi za kijamii
nchini kupitia miradi mbalimbali iliyo chini ya Benki hiyo.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Ms.
Bella Bird wakati wa kusaini hati ya makubaliano kuwa kutokana na
umuhimu wa kusaidia kaya maskini kupitia mradi wa TASAF, Benki ya Dunia
imetoa kiasi cha Dola za Kimarekani 200 sawa na shilingi za Kitanzania
Bilioni 440.
“Ili
Tanzania iweze kupambana na umaskini inahitaji kuhakikisha kaya maskini
zinapata huduma bora za afya na elimu ili kuweza kutimiza malengo yake,
Benki ya Dunia itaendelea kutoa msaada wa kifedha ili kufikia malengo
yaliyoainishwa na serikali,” amesema Ms. Bella Bird.
Aidha
Mkurugenzi huyo Mkazi amefafanua kuwa Benki ya Dunia inatambua umuhimu
wa kupambana na umaskini katika maendeleo ya nchi zote duniani ikiwemo
Tanzania katika kuleta maendeleo endelevu.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius
Likwelile amesema kuwa katika kipindi cha miaka hamsini ya ushirikiano
na benki ya Dunia katika mwaka wa fedha 2015/16 Serikali imeshuhudia
mchango mkubwa wa kifedha na kitaalam toka Benki ya Dunia.
“Napenda
kuchukua fursa hii kuishukuru Benki ya Dunia kwa msaada wake mkubwa wa
kitaalam na kifedha kwani mpaka sasa Serikali iko katika majadiliano na
Benki ya Dunia ili kuboresha bandari yetu ya Dar es Salaam,” amesema Dkt. Dkt. Likwelile.
Aidha
Dkt. Likwelile amezitaka Taasisi zote zinazopata fedha kutoka Benki ya
Dunia zitumie fedha hizo vizuri ili ziweze kuwanufaisha walengwa na
kuleta tija kwa Taifa.
Benki
ya Dunia inaisaidia Serikali ya Tanzania kwa kutoa ushauri wa kitalaam
pamoja na fedha kupitia miradi yake mbalimbali ili iweze kutekeleza
majukumu yake ikiwa ni pamoja na kupambana na umaskini hapa nchini.
No comments:
Post a Comment