Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo Juni 27 kwenda Gaborone,
Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wa Double Troika ya Asasi ya
Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit) utakaofanyika
kesho Juni 28, 2016.
Mhe.
Waziri Mkuu anamuwakilisha Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye
mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Gaborone (GICC).
Mkutano
huo utafunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Botswana Mhe. Lt. Jen. Seretse
Khama Ian Khama ambaye ni SADC, utajadili hali ya siasa, ulinzi na
usalama nchini Lesotho. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa
Makatibu Wakuu ambao utafanyika leo.
Pia
mkutano huo utahudhuriwa na Marais wa Afrika Kusini, Mwenyekiti
aliyetoka (outgoing chair) wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Mhe.
Jacob Zuma , Mhe. Jacinto Filipe Nyusi, Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji na
Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
Wengine
ni Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland ambaye ni Makamu Mwenyekiti
wa SADC, Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti
anayeondoka wa SADC.
Waziri
Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Aziz Mlima na
Maofisa wengine waandamizi.
No comments:
Post a Comment