Wednesday, 31 May 2017
Elimu zaidi inahitajika kuhifadhi mazingira nchini
WAKATI Mataifa mbalimbali
yanaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani yanayofikia kilele chake hapo
Juni 5, 2017, takriban hekta 372,000 za misitu hupotea kila mwaka nchini
Tanzania kutokana na shughuli mbalimbali. Mwandishi Beatrice Lyimo wa
Idara ya Habari – MAELEZO anaelezea zaidi. Kwa miaka mingi siku
ya Mazingira duniani imekuwa ikiadhimishwa kwa Wadau katika nchi
mbalimbali kuchukua hatua chanya zinazohusu mazingira. Siku hii pia
imekuwa ni sehemu ya kampeni ya utoaji elimu juu ya maswala
yanayojitokeza kuhusiana na mazingira.
Kauli mbiu katika maadhimisho ya
mwaka huu inasema “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira”
ikihamasisha jamii kuwa na urafiki endelevu na mazingira asilia ambapo
kila mtu anapaswa kutambua, kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa
mazingira asilia na kuhamasishana ili kuyatunza na kuyahifadhi.
Tanzania kama ilivyo kwa nchi
nyingi Barani Afrika na duniani kwa ujumla imeendelea kuathirika kwa
kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli
mbalimbali zikiwemo za kilimo, ufugaji, ujenzi n.k Mara baada ya
kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu aliagiza
kutofanyika kwa maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika ambayo yalizoeleka na
badala yake Watanzania waadhimishe siku hiyo kwa kufanya usafi. Mtazamo
wa wengi kuhusiana na maelekezo ya Dkt. Magufuli ulilenga zaidi katika
kubana matumizi mabaya ya fedha za Serikali.
Pamoja na mtazamo huo Mhe. Rais
aliona mbali zaidi, kwani usafi wa mazingira unasaidia kudhibiti
milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu, ambayo yanaigharibu
Serikali fedha nyingi zaidi ya zile ambazo zingetumika katika
kufanikisha maadhimisho hayo. Hivyo uamuzi alioutoa Mhe. Rais
utakumbukwa zaidi wakati huu ambapo nchi mbalimbali zinaadhimisha Siku
ya Mazingira Duniani.
Niko tayari kuondoka Barcelona- Iniesta
Nohodha wa Barcelona, Andres Iniesta bado ana ndoto za kuzeekea kwenye
Liga ya La Liga, huku akisema kwamba iwapo atatakiwa kuondoka yupo
tayari kufanya hivyo.
Iniesta mwenye miaka 33 mkataba wake unamalizika katikati ya mwaka 2018
na hatima yake imebaki njiapanda. Msimu huu alianza mechi 13 za ligi
msimu huu.
Kiungo huyo alisema bado ndoto zake ni kustaafu maisha ya soka akiwa
kwenye klabu yake ya Barcelona ambayo alijiunga tangu akiwa na miaka
12, akichezea timu ya vijana.
Mbowe amzuia Mbunge lucy kuchangia bungeni
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amesema
alipopata taarifa ya kifo cha Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Philemon
Ndesamburo alijaribu kumzuia mtoto wa marehemu, Lucy Owenya asichangie
bungeni lakini alishindwa.
Mbowe ameyasema hayo leo Jumatano wakati akilitangazia bunge kuhusu kifo cha Mwenyekiti huyo wa Chadema, mkoa wa Kilimanjaro.
Matukio Bungeni
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiingia bungeni huku akiongozwa
na askari wa bunge Bunge ili kuanza kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba
wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akisoma dua ya kuliombea Bunge
katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma
Mei 31, 2017.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Mhe.Dk.Medard Kalemani akiwasilisha Randama za Makadirio na Matumizi ya
Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha 38 cha
Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya
wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini
Dodoma Mei 31, 2017.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe katika kikao
cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Mhe.George Masaju akifuatilia jambo kutoka kwa Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk.Suzan Kolimba
katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma
Mei 31, 2017.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe.Prof Jumanne Maghembe akimskiliza Mbunge wa Mtama(CCM) Mhe.Nape
Nnauye katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini
Dodoma Mei 31, 2017.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali
mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge
la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge
katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma
Mei 31, 2017.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Mhe.Dk Charles Tizeba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika
kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31,
2017.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM)
Mhe.Ritta Kabati akiuliza swali katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba
wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
Mbunge wa Arumeru
Mashariki(CHADEMA) Mhe.Joshua Nassari akifurahi jambo na Mbunge wa
Momba(CHADEMA) Mhe.David Silinde katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba
wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA)
Mhe.Catherine Ruge akiuliza swali katika kikao cha 38 cha Mkutano wa
Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
Mbunge wa Iramba Mashariki(CCM)
Mhe.Allan Kiula akiuliza swali katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba
wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
Jumla ya Mizani 448 Yahakikiwa Mkoani Mwanza Ikiwa ni Maandalizi ya Ununuzi wa Pamba.
Wakala wa Vipimo (WMA)
Tanzania imeendelea na zoezi la utoaji wa elimu pamoja na uhakiki wa
mizani kwenye makampuni mbalimbali ya wafanyabiashara Mkoani Mwanza
katika Wilaya za Kwimba, Magu, Misungwi na Sengerema ikiwa ni
maandalizi ya msimu wa Pamba.
Akizungumza na Meneja wa Wakala wa
Vipimo Mkoani Mwanza Bwana Hemed Kipengele alisema jumla ya mizani
448 tayari imekaguliwa kutokana na makampuni manne ambayo tayari
yamekagulisha mizani yake na imekutwa ikiwa sahihi ambayo ni ICK (T)
LTD ambao walikuwa a mizani 184, SM HOLDING wenye jumla ya mizani 85
pamoja na NYANZA COTTON ambao walikuwa na mizani 179. Meneje
aliongezea kuwa zoezi hili la utoaji elimu pamoja na uhakiki wa mizani
itakayotumika kununulia Pamba linaendelea kwa Mikoa yote inayolima
Pamba ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera, Tabora pamoja na Mara.
Bwana Kipengele alisema
wanatarajia kutembelea jumla ya vijiji 101 ambavyo vina jumla ya vituo
vya kuuzia Pamba 150 ili waweze kutoa elimu na kufanya kaguzi za
kushutukize kwa wanunuzi wa Pamba ili kuona kama mizani waliyopima na
ikaonekana ni sahihi itaendelea kununua Pamba ya wakulima kwa vipimo
sahihi.
Meneja Kipengele aliwasihi
baadhi ya wakulima wanaolalamikiwa kuweka maji, kokoto pamoja na mchanga
kwenye Pamba kwa ajili ya kuongeza uzito waache tabia hiyo mara moja
sababu Sheria ya vipimo ipo na inafanyakazi kwa pande zote mbili muuzaji
na mnunuzi wote kwa pamoja hawatakiwi kufanya udanganyifu wowote katika
biashara.
Kipengele alisema Sheria ya
Vipimo Sura 340 inawataka Wakala wa Vipimo kuhakiki na kupiga chapa
vipimo vyote vinavyotumika katika biashara pia Wakala wa Vipimo
imeongeza na uwekaji wa sticker kwa kipimo kitakachokuwa
tayari kimehakikiwa ili iwe rahisi kwa wakulima kuona na kutambua mizani
iliyokaguliwa na kuruhusiwa kwa biashara kwa mwaka husika.
Man United ndio klabu yenye thamani kubwa Ulaya
Manchester United ndio klabu yenye thamani kubwa barani Ulaya ikiwa na thamani ya Yuro bilioni 3 kulingana na kampuni ya biashara ya KPMG.
Mabingwa hao wa kombe la Yuropa wanaongoza katika orodha ya thamani ya Kampuni ya KPMG, ikiwa mbele ya mabingwa wa Uhispania Real Madrid na Barcelona.
Utafiti huo uliangazia haki za kupeperusha matangazo, faida, umaarufu, uwezo kimchezo na umiliki wa uwanja.
Katika utafiti huo uliofanyiwa timu 32, vilabu vya Uingereza vilitawala orodha hiyo vikijaza nafasi sita kati ya 10 bora.
Andrea Sartori ambaye ni mkurugenzi wa maswala ya michezo katika kampuni ya KPMG amesema kuwa kwa jumla thamani ya soka imekuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
''Huku hilo likielezewa kufuatia kuimarika kwa matangazo, operesheni za biashara za kimataifa, uwekezaji wa vifaa vya umiliki wa kibinafsi, vifaa vya kisasa pamoja na usimamizi mzuri ni vigezo muhimu vya ukuaji huo'', alisema.
Kuhusu haki za matangazo, ligi kuu ya Uingereza inaongoza ligi nyengine za Ulaya ijapokuwa ligi nyengine zimeweka mikakati kupigania mashabiki wa kimataifa.
Vilabu kumi bora vyenye thamani ya juu kibiashara
1.Manchester United -Euro3.09bn
2.Real Madrid - Euro2.97bn
3.Barcelona - Euro2.76bn
4.Bayern Munich - Euro2.44bn
5.Manchester City - Euro1.97bn
6.Arsenal - Euro1.95bn
7.Chelsea - Euro1.59bn
Ndesamburo amefariki Dunia leo
Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi juu ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe.
IGP Sirro atangaza dau la milioni 120
Siku kadhaa baada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani kutangaza zawadi ya
Sh. milioni tano kwa mwananchi ambaye atafanikisha kukamatwa kwa
watuhumiwa 12 ambao limedai wanajihusisha na mtandao wa mauaji
yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji, Basi hii Leo
Mei 31, 2017 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Sirro ameongeza dau hilo
mpaka kufikia shilingi Milioni 10.
Katika mkutano wake wa Kwanza na Vyombo vya Habari Jijini Dar es salaam
tangu aapishwe, IGP Sirro amewaambia waandishi wa habari kuwa Jeshi hilo
linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao.
Kwamujibu wa ripoti Polisi imepata picha za baadhi ya watuhumiwa na fununu za mahali wanapopenda kutembelea mara kwa mara.
Kamanda Lyanga aliwataja watuhumiwa hao pamoja na mwanzilishi wa mtandao
huo wa mauaji kuwa ni Abdurshakur Ngande Makeo, Faraj Ismail Nangalava,
Anaf Rashid Kapera, Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa.Wengine ni Shaban Kinyangulia, Haji Ulatule, Ally Ulatule, Hassan Uponda, Rashid Salim Mtulula, Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame.
Hata hivyo ripoti za jeshi hilo zinasema, waimegundua kuwa watuhumiwa hao hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga, kisiwa cha Saninga katka kijiji cha Nchinga na kijiji cha Mfesini kata ya Nyamisati pamoja na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga.
Marekani wafanya majaribio mfumo wa kutegua mabomu
Marekani kwa mara ya kwanza imefanikiwa kuufanya majaribio mfumo wake wa kudungua makombora ya masafa marefu ICBM kulingana na maafisa.
Mfumo huo wa ardhini uliwekwa katika kambi moja ya kijeshi mjini California na kudungua kombora la masafa marefu kulingana na kitengo cha ulinzi wa makombora MDA.
Pentagon imesema kuwa majaribio hayo yalikuwa yamepangwa muda mrefu uliopita, lakini yanajiri huku kukiwa na wasiwasi mkubwa na Korea Kaskazini.
Majaribio hayo yamefanyika baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la tisa mwaka huu.
Mkurugenzi wa kitengo hicho cha ulinzi wa makombora Admirali Jim Syring amesema kuwa jaribio hilo ni hatua muhimu.
''Mfumo huu ni muhimu kwa ulinzi wa taifa letu na jaribio hili ni thibitisho kwamba tuna uwezo mkubwa dhidi ya tishio'', alisema siku ya Jumanne.
Lilikuwa jaribio la kwanza dhidi ya kombora la masafa marefu kwa mfumo huo wa ardhini GMD.
Mfumo huo ulirushwa kutoka Kwajalein Atoll katika kisiwa cha Marshal juu ya anga ya Pacific, kitengo hicho kilisema katika taarifa iliotolewa.
Tuesday, 30 May 2017
Yaliojiri leo Bungeni Dodoma Mei 30 2017
Mwenyekitiwa Bunge la
JamhuriyaMuunganowa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha 37 cha
Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya
wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini
Dodoma Mei 30, 2017.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mbunge wa
Kaliua(CUF) Mhe.Magdalena Sakaya katika kikao cha 37 cha Mkutano wa
Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia Mhe,Prof.Joyce
Ndalichakoakijibumaswalimbalimbaliyawabungekatikakikao cha 37 cha
Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
WaziriwaNchiOfisiyaRaisUtumishinaUtawala
Bora Mhe.AngelinaKairuki akijibu maswali mbalimbaliya wabungekatikakikao
cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
NaibuWaziriwaAfya,MaendeleoyaJamii,Jinsia,WazeenaWatotoMhe.KhamisKigwangallaakijibumaswalimbalimbaliyawabungekatikakikao
cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
NaibuWaziriwa Mambo
yaNjenaUshirikianowaAfrikaMasharikiMhe.Dk.SusanKolimbaakijibumaswalimbalimbaliyawabungekatikakikao
cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
WaziriwaViwanda,BiasharanaUwekezajiMhe.
Charles Mwijageakijibumaswalimbalimbaliyawabungekatikakikao cha 37 cha
Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
WaziriwaFedhanaMipangoMhe.Dk.PhilipMpangoakisomaHotubayaMakadirioyaMapatonaMatumiziyaWizarayaFedhanaMipangokwamwakawaFedha
2017/2018 katikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini
Dodoma Mei 30, 2017.
MbungewaVitiMaalum (CCM)
Mhe.FaidaBakarakiulizaswalikatikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa
Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
MbungewaVitiMaalum (CCM)
Mhe.AminaMollelakiulizaswalikatikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa
Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
WaziriwaHabari,Utamaduni
,SanaanaMichezoMhe.Dk.HarrisonMwakyembe akizungumza jambo naNaibu wake
Mhe.AnastaziaWambura katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11
leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
WaziriwaNchiOfisiyaWaziriMkuuSera,Bunge,Ajira,Kazi,VijananaWatuwenyeUlemavuMhe.JenistaMhagamaakijadilijambonaMbungewaIringaMjini(CHADEMA)
Mhe.PeterMsigwa katika kikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11
leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.GeorgeMasaju akifafanua jambo katika kikao
cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11leoMjini Dodoma Mei 26,
2017.Kushoto
kwakeni Waziri waNchi Ofisi yaWaziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,VijananaWatuwenye UlemavuMhe.JenistaMhagama naKulia niNaibuWaziri waNishati naMadiniMhe.Dk.MedardKalemani.
PichazotenaDaudiManongi,MAELEZO,DODOMA.
Ziara ya Makamu wa Rais mkoani Mara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, anatarajia kufanya ziara rasmi ya siku tatu kuanzia tarehe 05
Juni, 2017 Mkoani Mara.
Kwa mujibu wa ratiba ya Mkoa, Mhe Samia atatembelea Wilaya ya Tarime,
katika Kituo cha Afya cha Nyamwaga kinachojengwa na wananchi kwa msaada
wa Mgodi wa Acacia North Mara.
Pia, Mhe. Makamu wa Rais atapata fursa ya kutembelea Bonde la Mto Mara
kunakokusudiwa kuanza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari.
Mchana siku hiyo hiyo atafanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha
Bisarwi; katika eneo hilo kunakusudiwa kujengwa kiwanda cha sukari.
Aidha tarehe 6/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais ataenda Wilaya ya Serengeti
ambapo ataweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Wilaya; mchana
atafanya Mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Mbuzi, Mugumu mjini.
Tarehe 7/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais atakuwa Musoma ambapo ataweka jiwe
la msingi kwenye barabara ya km.9.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami
katika Manispaa ya Musoma. Pia atatembelea kiwanda cha Samaki cha Musoma
Fish Processors (T) Ltd na kufanya Mkutano wa Hadhara katika uwanja wa
Mukendo Musoma Mjini.
Mwita Waitara:Asilimia kubwa ya majibu Mawaziri ni uongo
Mwita Waitara Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) leo aliwashambulia mawaziri wa Rais Magufuli kwa kueleza kuwa majibu yao asilimia kubwa ni ya uongo,
Mwita ameelekeza mashambulizi hayo leo bungeni wakati alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kudai kuwa majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliani, Isack Kamwelwe ni asilimia tano tu ya swali lake na asilimia 95 ni uongo.
“Mimi ni mwalimu wa hisabati na kemia nimekuwa nisahihisha mitiani ya serikali na kama ningekuwa nasahisha mitihani ya mawaziri wewe ningekupa asilimia tano tu kati ya mia majibu niliyouliza imejibiwa asilimia tano tu yaliyobaki ni uongo.
“Inaonesha waziri hauna taarifa sahihi ya miradi ya maji ya kata nilizozitaja katika swali la msingi Je, huko tayari sasa uniletee taarifa sahihi.
“Je, kwa sasa hupo tayari nikukutanishe na akina mama ambao wanakumbana na adha ya kutafuta maji na kulazimika kununua maji kwa sh. 500 kwa ndoo ili uweze kusikiliza kilio chao juu ya kukosekana kwa maji?” alihoji Waitara katika swali lake la nyongeza.
Awali katika swali la msingi Waitara alitaka kujua serikali itakamilisha lini miradi ya maji ya kata za Chanika, Kipunguni na Majohe ili wananchi wa kata hizo na maeneo ya jirani wapate maji ya uhakika.
Matajiri Walivyomiminika na Magari ya Bei Mbaya kmzika Ivan wa Zari
watu wengi walikuwa wakiomboleza kifo cha Ivan Semwanga,
matajiri wakubwa na watu maarufu katika jiji la Kampala, waliitumia
fursa hiyo kujitokeza na kuonyesha magari yao ya bei mbaya.
Wakati ibada ya mazishi ya Ssemwanga iliyofanyika katika Kanisa la
Mtakatifu Paul la Namirembe mchana huu, matajiri wengi walijitokeza
katika msururu mrefu ambao ulisababisha msongamano wa magari katika
barabara ya Namirembe.
Pamoja na magari hayo kuwa ya bei kubwa, mengi yalikuwa na majina ya
wamiliki wake badala ya namba za usajili na hivyo kuwa kivutio kikubwa
kwa watu waliohudhuria mazishi hayo.
Matajiri maarufu kama Jack Pemba, Lwasa, Mugisha na mwanamuziki Bebe
Cool, walikuwa miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria ibada hiyo.
Ivan Semwanga alifariki katika Hospitali ya Biko Academy nchini Afrika
Kusini, Alhamisi wiki iliyopita kutokana na ugonjwa wa moyo na anazikwa
leo nyumbani kwao Kayunga.
Subscribe to:
Posts (Atom)