Na: Lilian Lundo – MELEZO – Dodoma.
Wabunge Wanawake, wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameadhimisha miaka 40 ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) kwa kufanya Mazoezi ya Viungo vya Mwili katika Viwanja
vya Jamhuri vilivyopo Mjini Dodoma.
Akiongea na Vyombo vya Habari
alfajiri ya leo, mara baada ya kumaliza mazoezi hayo, Naibu Spika, Dkt.
Tulia Ackson amesema kuwa wameamua kuadhimisha miaka 40 ya CCM kwa
kufanya mazoezi kutokana na mazoezi humpa mtu furaha, upendo pia
yanaunganisha watu.
Aliendelea kwa kusema kuwa,
kufanya mazoezi kuna punguza maambukizi ya magonjwa yasiyoambukiza
hivyo ni vyema kila mmoja kufanya mazoezi kama ambavyo Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inavyosisitiza juu ya
watanzania kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa hayo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa
imezoeleka katika jamii ya kitanzania kuona wanaume ndio washiriki
wakubwa wa michezo na mazoezi lakini ukweli ni kwamba wanawake ndio
wanaohitajika kufanya mazoezi zaidi kutokana na kuwa katika hatari kubwa
ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa kuliko wanaume.
“Ni wakati wa Watanzania
kubadilika na kuwashilikisha watoto wa kiume kufanya kazi za nyumbani
ili watoto wa kike nao wapate nafasi ya kushiriki michezo au mazoezi
kama ilivyo kwa watoto wa kiume,” alisema Anastazia Wambura.
Nae, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema kuwa, mazoezi yamemsaidia
awe na afya njema kutokana na kuwa mshiriki mzuri wa kufanya mazoezi
kila siku.
Vile vile Mabula amesema kuwa,
kufanya mazoezi kumemfanya aonekana kijana zaidi ya umri aliona, hivyo
amewataka wanawake kumuunga mkono Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa
kupanua wigo wa kufanya mazoezi.
No comments:
Post a Comment