Kwa siku kadhaa, kumekuwa na tuhuma zinazoelekezwa kwa Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, PAUL MAKONDA. Tuhuma hizo zimeanza kutolewa mara baada ya
Mkuu huyo wa Mkoa kuasisi mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ambayo
yameshika kasi sasa baada ya Rais MAGUFULI kumteua ROGERS SIANGA kuwa
kamishna Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini. Miongoni
mwa tuhuma hizo ni pamoja na;
1. Kutumia Jina lisilo lake la PAUL CHRISTIAN ambapo mwenye jina hilo ni
Mtangazaji wa Radio huko Tabora. Kwa mujibu wa tuhuma hizo, PAUL
MAKONDA majina yake halisi ni DAUDI ALBERT BASHITE. Jina la PAUL
CHRISTIAN lilikuja baada ya MAKONDA kutumia cheti cha mwenzake ili
aingie Jeshi la Polisi kwa vile yeye alifeli mtihani wa kidato cha nne.
Kwa vile PAUL CHRISTIAN halisi alifaulu division One, Busweru Sekondari
na kupangiwa Tabora Boys ambako alishindwa kuendelea na masomo ya kidato
cha tano kwa kukosa ada, MAKONDA akatumia cheti hicho kujiendeleza
kitaaluma. Tuhuma hizi zimezushwa na MANGE KIMAMBI ambaye mpaka sasa
ameshindwa kuweka ushahidi wa hoja zake.
2. Kununuliwa na wauza madawa ya kulevya gari la kifahari aina ya LEXUS
lenye thamani ya zaidi ya milioni 400.....Tuhuma ya Bungeni
3. Kumnunulia mke wake gari ya kifahari aina ya Benz lenye thamani ya
zaidi ya milioni 500 na kumkabidhi wakati wa sherehe ya siku yake ya
kuzaliwa...Tuhuma ya Bungeni
4. Kununua Appartment Viva Tower, Dar es Salaam....Tuhuma ya Bungeni
6. Kujenga jengo la ghorofa huko Mwanza ambalo limekamilika ndani ya
mwaka mmoja. Hata hivyo watoa tuhuma hizi waliingia mkenge baada ya
kuweka picha ya jengo ambalo ni Hotel iliyopo Kigoma.
7. Kusafiri kwenda Marekani na Ufaransa na kukaa siku 21 huku akipanda
ndege Daraja la Kwanza ambapo gharama ya nauli kwa yeye na mkewe ni Dola
za Kimarekani 14,000 kwenda pekee. Kwamba, kwa mshahara wa Mkuu wa
Mkoa, usingetosha kugharamia safari hiyo.....Tuhuma ya Bungeni
8. Kumpangishia nyumba ya kifahari AGNES MASOGANGE eneo la Makongo, Dar
es Salaam kwa vile ni mpenzi wake na ndio maana hakumtaja kwenye orodha
ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya......Tuhuma ya Wema Sepetu.
9. Kukarabati jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam bila
kufuata taratibu za manunuzi kwa gharama ya Milioni 400.....Tuhuma ya
Bungeni
10. Kumpigia simu Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya na kumtishia kuwa
yeye pamoja na wabunge wengine kama PETER MSIGWA, JOSEPH MBILINYI aka
SUGU, HALIMA MADEE, JOSEPH KASHEKU aka MSUKUMA atawashughulikia na
kwamba wabunge hao si lolote, si chochote.....Tuhuma za Bungeni.
11. Tuhuma ya kumporomoshe matusi Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Jambo
Leo baada ya kumuuliza swali kuhusu tuhuma za kutumia cheti kisicho
chake cha kidato cha nne.........Tuhuma ya Jambo Leo
Tuhuma ni nyingi na naamini wadau mtaongezea na mimi nitaedit uzi huu
ili kuleta mtiririko sawia. Hata hivyo, pamoja na shutuma hizo
kuporomoshwa juu yake, PAUL MAKONDA aliamua kutumia busara ya kukaa
kimya ili kuepusha mijadala isiyohitajika na hivyo kumtoa kwenye
harakati za kupambana na madawa ya kulevya.
Akiongea kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa hewani na
Clouds FM Radio, Mtangazaji wa kipindi hicho, BARBARA HASSAN ametoa
taarifa kuwa amempigia simu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam PAUL MAKONDA
na kumuomba ajitokeze kupitia kipindi hicho na kujibu tuhuma dhidi yake.
Habari njema ni kwamba, PAUL MAKONDA amekubali wito huo na kwamba kesho
tarehe 23 Februari 2017 atakuwa hewani 'LIVE' kuanzia saa 12.30 Asubuhi
kupitia KAKAKUONA na kuendelea hadi mwisho wa kipindi cha POWER
BREAKFAST cha Clouds FM Radio.
No comments:
Post a Comment